ANAYE SHITAKIWA PAMOJA NA PAPA MSOFE KWA MAUAJI AWACHOMA POLISI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mshtakiwa Makongoro Nyerere anayekabiliwa na kesi ya mauaji pamoja na Mfanyabiashara maarufu Abubakar Marijan [50] maarufu kama Papaa Msofe, amedai mahakamani kuwa amebambikiwa kesi hiyo.

Kadhalika alidai kuwa mahakama ikipitia jalada la kesi hiyo itabaini kwamba amebambikiwa kesi hiyo.

Nyerere alitoa madai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Hellen Riwa.

“Mheshimiwa hakimu, mahakama ikilipitia jalada la kesi hiyo kwa umakini, utabaini kwamba mimi sikuhusika na mauaji, nimebambikiwa baada ya askari polisi kuniomba rushwa ya Sh. milioni 8... nilipowakatilia kuwapa wakaamua kunipa kesi hii,” alisema Nyerere.

Alidai kuwa pamoja na mawakili wa upande wa Jamhuri kuwa ni wasomi wazuri, lakini wanafanya mambo yao tofauti na elimu waliyonayo na wanasabisha ateseke mahabusu bila sababu.

Hakimu Riwa alisema kwa kuwa upande wa Jamhuri umedai upelelezi bado haujakamilika, kesi hiyo itatajwa Oktoba 31, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa washtakiwa wote kwa pamoja walimuua kwa makusudi Onesphory Kituli, kinyume cha kifungu cha 196 cha Kanuni za Adhabu sura ya 19 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka, 2002. 

Ilidaiwa kuwa, Oktoba 11, 2011, nyumbani kwake Kituli, Magomeni Mapipa, wilayani Kinondoni washtakiwa walitenda kosa hilo. 


Hata hivyo, kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi upalelezi utakapokamilika kesi yao itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.


Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad