HIKI NDICHO KINACHOENDELEA KWENYE MSIBA YA BABA MZAZI WA WEMA SEPETU HUKO SINZA JIJINI DAR

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wema Sepetu akiwa katika hali ya majonzi baada ya kufiwa na baba yake mzazi




Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu.
  

Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori jijini Dar.



Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema.

Ndugu wa karibu wa marehemu akiwa na simanzi nzito
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki asubuhi ya leo.
Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya familia ya marehemu Balozi Sepetu.
Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto wa Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini Marekani, lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku ya Ijumaa.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Maskini pole Wema na familia yote ya Sepetu!

    ReplyDelete
  2. Poleni jamani familia ya sepetunga. ingawa ni kipindi cha majonzi mimi kama fan wa Wema nimefurahi sana kujua kuwa Wema ana dada wakubwa wazuri. Love you SEPETUNGA's DAUGHETR. na wazazi wenu wamewapa ajina mazuri sana. TUNNU, NURU, SUNNAH and WEMA. What a beutful names. RIP Mzee Sepetu. Mwenyezi mungu akupumzishe kwa amani.

    ReplyDelete
  3. Polee mungu atawafariji mdogowangu yote ni mapito

    ReplyDelete
  4. Pole sana kw yaliyokusib@Wema. Mungu amrehemu huko aendako apumzike kw aman#Amina

    ReplyDelete
  5. pole sana wema tuko pamoja katika wakati huu mgum

    ReplyDelete
  6. Pole sana madam,inshallah allah atawapa moyo wa faraja ktk kipind hchi kigumu....rip baba yetu....love u wema aka future mrs wa diamond

    ReplyDelete
    Replies
    1. duuh watu mashabiki hadi ukolezee mrs diamond. RIP Mzee Sepetu

      Delete
  7. pole sana mama sepetu c wanao tunakupenda sana mu akurehem r.i.p sepetu baba its me platnum

    ReplyDelete
  8. pole wema mwaya

    ReplyDelete
  9. We love Wema na tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu. Mungu awe pamoja nanyi pia Amen

    ReplyDelete
  10. pole sana wema,tupo pamoja katika msiba huu

    ReplyDelete
  11. pole kipenz wema ndo kaz ya mungu muombe tu yeye akupe nguvu yakuweza kustahimili yote haya pia muombe tu mzazi wako

    ReplyDelete
  12. wewe baba hamza aqcha uchoko dini kitu gani acha kuwaingilia watu na mipango yako kila kitu dini ...pole wema

    ReplyDelete
  13. Pole sana Wema Mungu awatie nguvu kwa kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  14. pole sana Wema Mungu akupe nguvu R.I.P baba yetu mpendwa

    ReplyDelete

Top Post Ad