AZAM TV WAMEJIPANGA SAWA SAWA ..KUANZA KURUSHA MATANGAZO MWEZI UJAO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kampuni ya Azam TV inatarajia kuanza rasmi matangazo yake mwezi ujao. Azam TV itakuwa ikitoa huduma ya matangazo ya TV ya dijitali kwa kutumia satellite ikiwa na king’amuzi chake ambacho tofauti na vingine itakuwa na malipo ya aina moja tu.

Cameraman wa Azam TV akiwa kazini
Ikiwa imeanzishwa mwaka huu pekee, Azam TV imepanga kupanuka zaidi na kuzifikia nchini nyingi za Afrika. Imedai lengo lake ni kuwa na vipindi vya aina mbalimbali kutoka channel za ndani na nje vinavyozifaa familia na watu wa kila rika.
IMG_4592
Pamoja na kuwa na channel zingine zipatazo 50, Azam TV itakuwa na TV zake tatu ambazo ni Azam One itakayokuwa ikionesha vipindi vya Kiafrika hasa vya Kiswahili, Azam Two itakayokuwa ikionesha channel za kimataifa ambapo vipindi vingine vitatafsiriwa kwa Kiswahili.
1383579_224622007704048_940194191_n
Pia kutakuwepo na channel ya Sinema Zetu ambayo itaonesha filamu za Tanzania saa 24.
Kampuni hiyo imejenga studio mbili kubwa zilizopo Tabata ambapo hadi January 2014 zitaanza kurekodi vipindi vya ndani na vya maongezi (talk shows).
IMG_4565
Wafanyakazi wa Azam TV wakiwa pamoja na waandishi wa habari waliotembelea studio zao

-BONGO5



Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HONGERA AZAM.Sasa tunasubiri na Azam Airways.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Baada ya Azam airways itakuja Azam train.
      tunaomba train hii iende mikoa ya kusini eg Mtwara, Lindi etc

      Delete
  2. Umeona , me nasomea pilot huku nasubiri kuwa pilot Azam airways nahisi soon hatakuwa na private jet yake

    ReplyDelete
  3. Aisee bora sana. Haya mastartimes mabovu,mara masaa matatu channel zimekata tutayatupa kuree. Safi sana

    ReplyDelete

Top Post Ad