LULU : " SITAKI KUOLEWA MUDA WA KUOLEWA HAUJAFIKA"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekataa kabisa suala la kuolewa kwa sasa akidai moyo wake haupo tayari kwa tendo hilo.

Lulu alifunguka hayo Jumatatu iliyopita katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa kupitia Runinga ya East Africa ambacho humpa nafasi staa kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake na sanaa kwa jumla.

Wakati mahojiano hayo yakiendelea, mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho anayefahamika kwa jina la Muba, alimtupia Lulu swali ambalo lilimtaka aeleze utayari wake endapo mtu akijitokeza na kutaka kumuoa.

“Sitaki kuolewa kwa sasa, muda wa kuolewa haujafikia. Ukifika nitafanya hivyo lakini kwa sasa sipo tayari kuolewa,” alisema Lulu.
Aidha, Lulu alikiri kuwa licha ya kutokuwa tayari kuolewa lakini amekuwa akipata usumbufu mkubwa wa kutongozwa na wanaume. Aliainisha kuwa alikuwa akitongozwa kabla na baada ya kutoka Segerea alipokuwa akishikiliwa kwa kesi ya kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba.
 “Watu wananitongoza sana, walikuwa wakifanya hivyo kabla hata sijaingia China (gerezani Segerea) na wameendelea kufanya hivyo hata baada ya kutoka,” alisema Lulu na kuongeza:
“Siwezi kuwakubalia sababu sipo tayari kuolewa kwa sasa…muda wa kufanya hivyo haujafika.”
Kuhusu suala la kudaiwa kutembea na bosi wa Kampuni ya Proin Promotion ambayo inamsimamia kisanii kwa sasa, Lulu aliruka viunzi na kudai taasisi hiyo inamlea kama mtoto wa familia na siyo vinginevyo.
Alisema hata madai yanayoelekezwa kwake kuwa Proin wamempa gari na nyumba kama sehemu ya kuhongwa na bosi wa kampuni hiyo, hayana ukweli wowote kwani yeye anafanya kazi kama msanii chini ya kampuni hiyo na hakuna kitu cha ziada.
“Hahahaha! Salama (mtangazaji) acha mambo yako bwana… mimi nipo chini ya Proin kwa sasa kwa kipindi flani ambacho nimesaini nao mkataba. Wananilea kama msanii wao, hakuna cha ziada,” alisema Lulu.

Akiendelea kubwabwaja maneno ndani ya kipindi hicho, Lulu aliweka wazi kuwa alikuwa akishindwa kuanika penzi lake na marehemu Kanumba kwa kuwa muda muafaka ulikuwa haujafika na kudai waliishi kama mtu na baba yake kabla hawajawa wapenzi, wakawa wapenzi na mauti yakamkuta Kanumba kabla hawajalianika penzi lao.

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama hutaki kuolewa wache waume za watu maana una mlolongo wa waume wanaokutongoza uliwapate kufuli lako

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wa kukuoa umempata uwongo mtupuuu wasichna wa mjni waongo hatujui moyoni mwako shoste unafkri kuolewa rahisi,

      Delete
  2. Uache umalaya na kuiba waume za watu hiyo boss wako ni kweli unatembea naye

    ReplyDelete
    Replies
    1. akhaa!!!! siwezi kuuoa huyu naogopa kufa mapema. kama..........!

      Delete
    2. Bora umefunguka mianaime Ina roho ngumuuuu mtu katembea na msululu Wala hawaogopi kutumbukiza miboo yao.Ukimwi unatesa mno.

      Delete
  3. LisichAna hili malayaaaa likifikwa 25 naona Wanaume watafika Mia .

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli yaliyo baki ni mapumba ovyoooooo, rudi shule

      Delete
  4. Sasa hata huyo mwanaume atakaeyekuja kukuoa anaweza kweli kumwambia mtu eti ameo mwanke watu wakamsiliza kweli? Kwa maana nikujuavyo hauna mahali pamebaki hapaja chezewa vibaya sasa sijui huyo mwanaume atakuolea nin sipati picha hapa !!

    ReplyDelete
  5. Kukuowa wewe nisawasawa ma kununu

    wa gari Bea ijini

    ReplyDelete
  6. na hutopata wa kukuoa abadan asilan labda umrudie mola wako

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. huyo hana lolote yote yameliwa lol!!!!

    ReplyDelete
  9. kabla ya kutaka kuua mwingine muombee mwenzio kwanza R.I.P KANUMBA. inaonekana umemsahau kabisa foolish girl

    ReplyDelete
  10. Weee ufikili watu hawaogopi kufa..nani atakubali kukuoa

    ReplyDelete

Top Post Ad