DIAMOND ATOA SIRI 5 ZA KUMRUDIA WEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja


MKALI wa songi linalotamba runingani na redioni ndani na nje ya Bongo la Number One, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kuanika siri tano za kurudiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

Wiki mbili zilizopita, wakiwa Hong Kong, China, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viliripoti kurudiana kwa Diamond na Wema waliomwagana takriban mwaka mmoja uliopita ambapo staa huyo wa Bongo Fleva aliibuka na kukanusha vikali akidai kuwa picha zinazomwonesha yuko na Wema ni za Filamu ya Temptations.

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa dakika ishirini katika mahojiano maalum jijini Dar mara tu baada ya kutua kutoka China Jumatano iliyopita, Diamond alikiri kufaidi penzi la Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.

Diamond alisema kuwa, Wema ndiye aliyetangulia kwenda China ambapo yeye aliungana naye siku kadhaa baadaye akitokea kwenye shoo nchini Malaysia.

SIRI YA KWANZA
Akianika siri za kujikuta mikononi mwa mwigizaji huyo mwenye mashabiki wengi zaidi katika tasnia ya filamu za Kibongo, Diamond alisema kwanza ni ukarimu aliopewa na mrembo huyo.

Alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.

“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile.

Akaongeza: “Kwa mazingira yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume aliyekamilika arudishe moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.


“Kiukweli nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.”

SIRI YA PILI
Diamond alisema baada ya mapokezi ya nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya nyota tano (five stars) ambapo huko alipatiwa huduma ‘klasiki’ na kujiona kama yupo kwa mama Nasibu vile.

SIRI YA TATU
Alifunguka kuwa kitendo cha Wema kuwa mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni hadi akapazoea nacho ni siri nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’.

SIRI YA NNE
Alisema kuwa mwanadada huyo alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa kimapenzi) hivyo haikuwa rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo penzi jipya linachipuka, akajikuta akiogelea naye. 

SIRI YA TANO
Diamond alisema kuwa bado ana ndoto ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye anajua kuwa alishamwambia lengo lake juu ya kupata naye uzao hivyo katika nyakati za kukutana kwao anaamini ndoto itatimia.

HAKUNA CHA FILAMU
Alipoulizwa juu ya madai kuwa walikuwa wakirekodi filamu, Diamond alifunguka kuwa hakuna cha filamu wala sinema na kama kuna mtu anasubiri filamu atakaa sana.

“Naomba nikiri kuwa kweli zile picha hazikuwa za filamu wala nini bali ndivyo hali halisi ilivyokuwa kati yangu na Wema kule China.
“Pia naomba niseme kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi uliishia China na sasa hivi tumebaki kama kaka na dada na ni ruksa kila mtu kumtumia mwenzie katika kazi mbalimbali kama ataona kuna ulazima wa kufanyika hivyo,” alisema Diamond.
Hii ni mara ya kwanza kwa Diamond au Sukari ya Warembo kukiri kuwa kweli alirudisha penzi lake kwa Wema walipokuwa nchini humo wakijiachia.

PENNY HANA CHAKE?
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Diamond, ukifuatisha simulizi hiyo ya mapenzi kati ya msanii huyo na Wema, ni dhahiri kuwa mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ hana chake kufuatia usaliti huo.


Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.

GPL

Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Penis unamoyo...cdhan km unamapenzi ya dhat kwa diamond!?! Kwa hicho alichokiri anakuonyesha waz HAKUPENDI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mali zoteee nimechuma nae.siziachi.

      Delete
  2. Duuuuuuuh...wajameni!

    ReplyDelete
  3. Diamond na Wema= Mtuache tufanye yetuuu lol

    ReplyDelete
  4. Atanteeeee tana....

    ReplyDelete
  5. kazi kweli kweli,chezea mapenzi wew?

    ReplyDelete
  6. diamond kafulia kwenye upande wa media so anaona akimrudia wema atakua kwa hewa kila mda,,,nimeamini ya waswahili kua walionana uchi mchana si rahisi kuachana,,,,,

    ReplyDelete
  7. Ushenz Tu huu hamna lolote

    ReplyDelete
  8. pole peny unaroho ngumu kama mkaanga sumu huchoki tu au hela dai huwa anakupa nyoooo...Tunda la msimu

    ReplyDelete
  9. mjinga cna dai kuwab
    adilisha makahaba kanaona cfa ? Nyoooh!

    ReplyDelete
  10. Unalo Pensel wino umeisha, labda jaribu kumpa dimond mkundu uenda akatulia, nawatuache tulale (wema+dimond)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo la penseli anatumia nguvu nyingiiiii kufuga kunguru, fuga kuku penny,kunguru toka lini akafugika?wema na diamond ni masharobaro wanawezana Kwa kila kona.

      Delete
  11. Mi nshajua kama diamond wanampapatakia kwa kua ye ni superstar,ivi angekua na maisha kama yangu unadhani wangukua wanamzimia hivo????

    ReplyDelete
  12. Mdau,ndo unasanuka leo, huo ndo ukwel wenyewe,joket anatuzingua et jamaa anajua kutongoza,mara anajali, wap?yan dunia ya leo ukiwa staa umemaliza kilaki2,utaonekana unaakil,unajua sana mapenzi,umesoma kila mwanamke atakusifia,na utawagonga wanawake wazur wote unaowajua hapa tz

    ReplyDelete
  13. Wemaaaa luv u sanaaa.....tim Wema ooyeeeeeeeee,!!!!!!!!

    ReplyDelete
  14. Ukweli huwa haujifichi hata siku moja................rahaje

    ReplyDelete
  15. kila mmoja anadhambi zake na dhambi hazifanani hata siku moja, ww unae mjudge huyu dada inaweza kua umetembea na mke wa mtu au mme wa mtu ni dhambi pia umetukana,umesengenya,umefanya uovu tofauti na wa kwake.................na inawezekana dhambi yako ni mbaya kuiko hata ya kwake so guys think on ur life not some one life

    ReplyDelete
  16. hamna ubishi, wema na diamond wanapendana, wanapendezana, wanakick, na aliyosema diamond duuh!!! penny huna lako mamii, kusanya shuka lako la maua ulilolinunua manzese basi uende zako, sasa sijui utatuambia unakaa kwa diamond for what reason? because u love him or because mawifi loves u? hivi kusoma hujui hata picha pia huzioni? hivi unawazazi kweli? na wanaposikia na kusoma habari kama hizi wanajisikiaje? na wanakushaurije? imefika wakati hebu jitambue, angalia wapi ulipodondoka simama jipanguse, uende zako, wakati wa diamond kuwa na wewe umepita, na kwa aliyoyaongea anataka kupata mtoto na wema unadhani wameachana? au ni wakuachana? diamond anaonyesha hana hata chembe ya mapenzi kwa penny na imebaki story, ktk wimbo wa MY NUMBER ONE kunasehemu ameimba NAMENGINE KADHALIKA MTOTO SI UNANIELEWA, HAPO HAPO ULIPOSHIKA UKIONGEZA KIDOGO MKE MWENZAKO UTAMUUDHI, Wema ameyafanyia kazi hayo maneno na kweli Penny umeudhika na kakupoteza ktk ramani ya mapenzi kwa diamond, na sasa WEMA NDIO NUMBER ONE. naweza kumpongeza wema kwani kafanya uanamke zaidi, mwanamke vitendo, kamshika DIAMOND NA AKAONGEZA KIDOGO yaliyotokea yakatokea. hongereni sana kwani penzi la kweli halijifichi

    ReplyDelete
  17. PENY kuma imeshasokotwa na kuachwa

    ReplyDelete

Top Post Ad