MELI ILIYONASWA NA ‘UNGA’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Stori:  Waandishi Wetu
WIKI iliyopita Jeshi la Polisi Kikosi Kazi cha Wanamaji Tanzania, walikamata shehena ya madawa ya kulevya ‘unga’ wenye thamani ya mabilioni ya shilingi zikiwa ndani ya meli.

Taarifa za uhakika zinadai kuwa meli hiyo ambayo ni mali ya Kampuni ya  Almansoor SA ya Iran ilikamatwa Jumanne iliyopita katikati ya bandari za  Zanzibar na Dar es Salaam.

Meli hiyo ilikamatwa baada ya askari waliokuwa doria kuilitilia shaka na  kufuatilia kwa karibu ili kujua ilikuwa imebeba nini.

Vyanzo vilivyokuwa katika eneo la tukio  vinasema kuwa meli hiyo ilikuwa na watu 12 na baada ya kupekuliwa ndipo walikuta kilo 201 za madawa ya kulevya aina ya heroine.

Watu waliokamatwa katika meli hiyo ni Mohamed Hassan (30), Abdul Nabii (30), Fahiz Muhamad (34) na  Rahi Baksh (30), wote raia wa Pakistani.

Wengine ni Abdulsamad Badreuse (47), Hazra Azat (60),
Nahimu Musa (25), Khalid Ally (35),  Kher Murad (38), Said Mohamed (34), Murad Gwaharam (38) na Ayub Hot (50) ambaye ni nahodha wa meli, wote raia wa Iran.

Meli hiyo ilikuwa na mtazamo wa kivuvi na lengo la wahusika ilikuwa wasishtukiwe kirahisi.
“Ilikuwa si rahisi kuigundua kama uwezo wako wa kufikiri ni mdogo lakini askari wetu wana akili sana na ndiyo maana meli ile ilihisiwa mara moja,” alisema mtoa habari mmoja kutoka jeshi la polisi.

Naye Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji Tanzania, ACP Mboje Kanga alisema ilikuwa ni kazi kubwa kuibaini meli hiyo ilikuwa imebeba nini lakini kwa kutumia mbinu za kiintelijensia waliweza kuitilia shaka na kuipeleka bandari ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Uwazi, unga huo ulikuwa utue katika maeneo ya Ilala jijini Dar ambapo baadaye ungesambazwa kila kona ya nchi ya Tanzania.

“Ndugu waandishi, Ilala kuna maeneo ambayo ni maarufu sana kwa biashara kama hiyo, ule unga ulikuwa upelekwe Ilala halafu upelekwe nchi nzima,” kilisema chanzo chetu.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa akizungumza na gazeti hili kuhusu madawa hayo, alisema kama yangefanikiwa kutua Dar na kusambazwa nchini watu milioni 3 mpaka 4 wangetumia, hasa vijana.

Kamanda Nzowa alisema meli hiyo ilitiliwa shaka  kutokana  na kutokuwa na utambulisho wa nchi husika, yaani bendera kama  meli zingine.

Akasema baada ya upekuzi waligundua  zaidi ya kilo 201 za heroin zenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 9.

“Mpaka sasa upelelezi unaendelea ili kubaini mwenyeji wao ambaye angewapokea Dar es Salaam ni nani maana kwa vyovyote yupo, tukimbaini amekwisha,” alisema Nzowa
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ingekuwa vyema kama mtampata huyo mwenyeji!!!

    ReplyDelete
  2. Acheni upuuzi wenu wenyeji mnawajua sana na huo mzigo wenu nyie viongozi na kama utue ilala inamaana mnamfahamu mwenye mzigo na hayo madawa mnayokamata mbona ha2oni mkiteketeza mnateketeza vipodozi 2 au ndo huwa yanaishia mikononi mwenu joto hasira

    ReplyDelete
  3. inaishia mikononi mwao halafu wanawapelekea wahusika kwa kuwauzia tena kwa siri, tumekwishaa, natamani Nyerere angeishi milele!

    ReplyDelete
  4. Wasenge tu hawa, wanavimbisha mabusha yao kwa ajili baba ni raisi, acheni usenge nyie..... mnajulikana mahanithi nyie, mnauwa watoto wa watu kwa tamaa za dunia mkifa mnazikwa na shuka tu kumamae zenu

    ReplyDelete
  5. Bilioni 9 ni noma huo unga unatakiwa ukachomwe mbele ya watu tena uwanja wa taifa

    ReplyDelete
  6. mashoga hawa wanavaa kanzu bila vhupi hapa. wauji kama nini hawa. balaa tu hawa pun=mbavu zao sana ha

    ReplyDelete
  7. bakari kitambulio12 February 2014 at 09:16

    kilo 201 za heroine? Watanzania hasa vijana kaaz ipo

    ReplyDelete
  8. mh mbona cjawai kuckia madawa ya kulevya yakiteketezwa? Maana kuwakamata ni kila cku mnawakamata

    ReplyDelete

Top Post Ad