"MSIMAMO WANGU, SAKATA LA POSHO BUNGENI"JOSHUA NASSARI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MSIMAMO WANGU, SAKATA LA POSHO BUNGENI.

Nimeona nukuu kwenye gazeti la nipashe la leo. Kimsingi ike nukuu si ya kwangu ni nineshazungumza na Mhariri wa jipashe Bw. Kwayu.
Sijui kama nukuu ile imewekwa kwa kukosea au kwa makusudi, wameahidi kurekebisha makosa lakini ni vyema nikaweka msimamo wangu hapa.

Kwa hali halisi ya maisha ya kawaida ya Mtanzania wa shilingi laki 3 ni fedha nyingi. Na taasisi ya Bunge ndiyo inayopaswa kuwapigania hawa watanzania ili vipato vyao vipande lakini taasisi hii siku zote imekubali kuwa upande wa serikali badala ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.
Fedha hiyo bado ni nyingi mno kama kipato cha mtanzania kinabaki kuwa hapo kilipo.

Kabla ya kupigania ongezeko ambalo linaweza wakati mwingine likawa na mantiki, ni vyema wabunge wakaifanya kwanza kazi yao ya kupigania maisha bora na maslahi bora kwa wananchi hiki hiyo mantiki yao kama ya kufanya mabadiliko ya posho ya shilingi elfu arobaini 40,000/= atakayolipwa mbunge iwapo ataugua akiwa Dodoma iweze kuonekana. Otherwise na sisi wabunge tutakuwa ni sehemu ya dhambi ya mateso na hali ngumu ya maisha ya watanzania ambao bado wanajifungulia sakafuni na hawana maji safi ya kunywa. 

Joshua Nassari (MB) na mjumbe wa bunge maalum la katiba.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. safi sn joshua nasari ndiyo faida ya elimu hiyo

    ReplyDelete
  2. Mhs Nassari umenena na tunataka watu kama nyie ndiyo mtuwakilishe, siyo yale yanayokwenda kule kwasababu ya matumbo yao, Mungu ayalaani hayajali maisha ya watu wengine.

    ReplyDelete
  3. na rais akikubali kuwaongeza posho nitamshangaa kuongeza mshahara kima cha chini laki tatu mlikataa katakata leo mbunge anapewa posho laki 3 kwa siku eti ndogo jama jaman hebu muwe na aibu mlo kwa siku hajui atakula nn wewe unapewa laki tatu unasema ndogo kweliiiiiii this is embarrassing wallah nimewachukia kupita maelezo

    ReplyDelete
  4. Inawezekana kabisa kwamba laki tatu hazitoshi! Lakini sasa, hatuna zingine! kwa hiyo anayeona haitoshi arudi nyumbani kwake kwenye hela nyingi!

    ReplyDelete
  5. km mtu hatakarud kwake baaac afu io laki3 kwa cku hamna haya nyie mavi kunuka mungu awe nanyi hzo hela mnapeda km mnazikwa nazo

    ReplyDelete

Top Post Ad