CCM YAKIRI INA MASLAHI NA SEREKALI MBILI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesisitiza msimamo wake wa kutaka kuendelea na muundo wa Serikali mbili huku kikiweka wazi kuwa kina masilahi makubwa na mfumo huo.

Kimesema suluhisho la kumaliza changamoto za Muungano siyo kubadili muundo wake na kuwa na Serikali tatu, bali ni kuufanyia maboresho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema: “Kimsingi CCM ndiyo waasisi wa Muungano na ina masilahi makubwa na mapana na Muungano huu kama waasisi pengine kuliko taasisi nyingi ndani na nje ya nchi yetu.”

Alisema licha ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kueleza bungeni sababu za Tume hiyo kupendekeza mfumo wa Serikali Tatu, chama hicho kinaamini kuwa suluhisho la kero za Muungano haziwezi kumalizwa kwa kubadili muundo wake.

“Kazi ya Warioba na Tume yake sasa imekwisha rasmi. Kwisha kwa kazi yao ni mwanzo wa awamu nyingine ya mchakato huu. Mwisho wa kazi ya tume hiyo siyo mwisho wa mjadala juu ya Katiba tuitakayo, bali ni mwanzo wa awamu nyingine mbili za mjadala mpana na maboresho kama siyo marekebisho ya kuondoa upungufu kwenye rasimu iliyowasilishwa. Awamu hizo mbili ni Bunge la Katiba na Kura ya Maoni.”

Alisema katika Bunge la Katiba kutakuwa na fursa nzuri ya kupima kama yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na maelezo ya ziada yaliyotolewa na Jaji Warioba yanaakisi maoni ya Watanzania walio wengi.

“Tuna imani na awamu mbili zilizobaki kwa kuwa zinahusisha wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge Maalumu la Katiba na nyingine kuwahusisha wananchi moja kwa moja, zitatumika vizuri kutupa jibu la nini matakwa ya Watanzania juu ya Katiba waitakayo,” alisema Nape.

Alisema chama hicho kinatambua umuhimu wa kuimarisha Muungano na kwamba njia pekee ya kuudumisha ni kufanya maboresho kwenye muundo wa Serikali mbili.

Akitolea mfano kero za Muungano, Nape alisema: “Hivi sasa tuna Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo ni ya Muungano. Moja ya malalamiko ya Zanzibar ni kwamba katika Serikali ya Muungano kuna baadhi ya mambo siyo ya Muungano ni ya Zanzibar.” Aliongeza: “Lakini unapozungumzia misaada na mikopo kutoka nje lazima ipitie kwenye dhana inayoitwa uhusiano wa kimataifa. Wao wanasema wizara ambazo siyo za Muungano zinakosa fursa ya kupata misaada na mikopo kutoka nje kwa sababu hazipo katika Muungano na hazifanyi kazi na wizara za Muungano.”

Alisema suluhisho la jambo hilo siyo Serikali tatu, bali ni kutenganisha uhusiano wa kimataifa na mambo ya nje, “Mambo ya nje mnaweza kulifanya kuwa la Muungano. Uhusiano wa kimataifa mkalitenga. Kila upande utakuwa na uhuru wa kuwa na uhusiano wake, hilo linaweza kufanyika hata kukiwa na Serikali mbili.”
-Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. asante nape weeeeeeeee ndo maana katibu wa ccm, ni kweli kinachotakiwa ni kuboresha vitu vya muungano wa serikali mbili na si kuleta serikali tatu. kama haiwezekani bac kila mtu kwao

    ReplyDelete
  2. Muunga Noooooooo!

    ReplyDelete
  3. Serikal 3 or 2, hazinisadii lolote kwnye maisha yangu, maendeleo kwngu yatakuja kwa kujituma mm mwenyewe so naona kero tu kila kukicha mizozo mizozo , pumbavu zenu nyie mafisadi wa nchii, MUNGU tembelea mafisadidi mmoja hadi mwngne wakumbushe kula kwa jasho kama ss wengine

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama unalijua hilo hakukua na sababu ya kukoment humu

      Delete
  4. Pumbavu kweli wewe nepi!
    Unayoyaongea kweli yanaaki ile division four yako ile!!!!

    ReplyDelete
  5. Pumbavu kweli wewe nepi!
    Unayoyaongea kweli yanaaki ile division four yako ile!!!!

    ReplyDelete
  6. Matusi ya nn huyo jamaa kaongea ukweli, bila kukaza ww mwenyewe utatoka kapa kwenye dunia hii, siasa haina maana yoyote kwa wananchi, wasenge nyie mnaoshabikia siasi bila kutumia akili

    ReplyDelete

Top Post Ad