KENYA NAO WATAKA SHERIA YA USHOGA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nairobi. Mbunge Irungu Kang’ata anaongoza juhudi za kundi lililoundwa la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini  Kenya. Sheria zilizopo zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela.

Huenda ikawa nchi inayofuata kwenye utata unaohusiana na haki za wapenzi wa jinsia moja, huku wabunge wakipanga kuwasilisha muswada bungeni kushinikiza Serikali kufanya juhudi zaidi kutekeleza sheria zilizomoza kupiga marufuku ushoga.

Kwa upande wao wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanasema shinikizo limeongezeka tangu nchi jirani ya Uganda ilipopitisha sheria dhidi ya mashoga mwezi uliopita.

Irungu Kang’ata ambaye ni mbunge kwa mara ya kwanza anaongoza juhudi za kundi lililoundwa majuzi la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya. Katika kampeni za wazi kabisa, mbunge huyo ameomba chama tawala kuelezea Serikali inachukua hatua gani kutekeleza sheria zilizopo dhidi ya mashoga.

Sheria zilizopo nchini  Kenya zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni kifungo  cha miaka 14 jela.

Kundi hilo linalopinga wapenzi wa jinsia moja  liliundwa majuzi wakati Rais wa nchi jirani ya Uganda Yoweri Museveni alipotia saini sheria dhidi ya wapenzi wajinsia moja mwezi Februari, licha ya shinikizo kutoka kwa nchi za Magharibi asitie saini.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WABONGO TAYALI TULISHATIA SAIN

    ReplyDelete
  2. Kama ilivyokuwa kipindi cha Sodoma na Gomora ndivyo itakavyokuwa kipindi karibia na mwisho wa dunia. Asomaye na afahamu.

    ReplyDelete
  3. Ofcoz sheria hizo zinatolewa na wanaume! Kenya wakitowa sheria hiyo wa Kenya wote wataenda jela , asilimia 95% ya wa Kenya ni magay u lesbian ndio usiseme! Jamani muachieni Mungu kazi yake, kama yeye Aliye waumba kawaacha waishi basi anamaana yake.

    ReplyDelete

Top Post Ad