MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGE LA KATIBA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dodoma, Tanzania. Mchungaji Christopher Mtikila amechafua hali ya hewa bungeni, hivi punde kwa kumtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Kificho amueleze ni kwanini tangu jana amekuw akimnyima nafasi ya kuzungumza bungeni.

Mchungaji Mtikila alisimama ghafla na kusema: Mwenyekiti kwanini unaninyima haki yangu ya kuzungumza, nataka kujua kwanini unaninyima haki ya kuzungumza. Kuzungumza ni haki yangu."


Mchungaji Mtikila amezungumza kwa jazba huku wajumbe wengine wakimzomea, lakini bila uwoga aliendelea kuzungumza na kusema yanayofanyika Mungu anapenda na yeye ana amini katika Mungu, lakini "Wewe Mwenyekiti inaonekana kuwa hupendi Mungu."

Wakati Mchungaji Mtikila akimwakia Kificho, Felix Mkosamali alilipuka na kumwambia mwenyekiti kuwa tangu jana pia anamnyima nafasi.
"Ninyi mmejipanga, kupitisha kanuni mbovu, alafu sisi wengine hamtupi nafasi," amesema Mkosamali.

Mwenyekiti Kificho aliwajibu kuwa kwa bahati mbaya wamekosa nafasi na hivyo wawe wavumilivu.

Kificho anatangaza utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge na wajumbe wanaotaka kugombea nafasi hiyo wametakiwa kuchukua fomu ya kugombea.

Bunge hilo limeahirishwa mpaka kesho na kanuni zitaanza kufanya kazi rasmi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. haya yetu macho na masikio mkitoana macho haya mkitoana masikio haya kz kwenu tunachotaka ni katiba ya miaka 100 ijato iliyo imara na nzuri

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio miaka 100 ni miaka 500,mpaka yesu arudi

      Delete
    2. BUNGE LINAHITAJI MAOMBI/ DUA ILI LIPATE KIBALI KWA MUNGU..La Sivyo hakuna Muafaka..kila siku tutasikia kioja kipya Na muda unazidi kupotea.

      Delete
  2. Bunge gani hili kila siku kughailishwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. wengi wao wanavirus kwa hiyo msiwalaumu....brains zao azifanyi kazi vizuri ..ikizingatia wameshazoea rushwa,sisi aitupunguzii kitu waneng'eneke lakini at the end watapata muafaka.

      Delete
  3. Tutaandamana paka dodoma au wadau mnasemaje? Wote wanaosumbua ni ma ccm pumbavu zao fyuuuuuuu8

    ReplyDelete
  4. khah miaka 500 hapana chezea

    ReplyDelete
  5. CCM imetoka wapi tena? wewe CHADEMA nini? maana ndio hawana adabu, sijui wamemtuma mtikila afanye fujo we akili yako kama haina akili mbulula we? watu wengine bwana wenzao wanachangia wao wanakunya.

    ReplyDelete
  6. huyu mtikila hana adbu

    ReplyDelete

Top Post Ad