PROF ISSA SHIVJI NA UBAKAJI WA MATAKWA YA UMMA KWENYE MUUNDO WA MUUNGANO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sijawahi kufundishwa na Profesa huyu anaeishi Amerika akighani sheria zake katika uga wa Pwani ya Azania, nimjenzi mzuri wa hoja za kisheria vilevile jamii ya kiswahili inamuamini kwa misimamo yake,


Baada ya Tanzania kuanza mchaato wa kupata katiba mpya ya Muungano, Prof Shivj alikuwa miongoni mwa watu wanaotazamiwa kulisaidia taifa kupata katiba bora kabisa ya "KIRAI", lakini katika hali isiyotegemeka, mamlaka zote za nchi zikamtelekeza, akawa sasa ni deiwaka tu msako wa katiba mpya, akionyesha kuheshimu misimamo ya uuma.

Mnyukano wa kimaslahi kati ya Chama cha Mapinduzi na UMMA wa Watanzania, umemrejesha tena Issa Shivji mbobevu wa sheria za kiutawala, lakini akija kwa nadharia ya kusigina matakwa ya umma,

Yule Issa Shivji aliyekuwa mtetezi wa matakwa ya umma, leo amekuwa mpiga zumari wa Lumumba. Issa Shivji anafikiri Watanzania ni wajinga kiasi cha kumfuata kila akifanyacho, vikao vyake vya ikulu wiki jana kwamalengo ya ghiriba wa umma havita saidia Watanzania kudai Muungano wao BORA kabisa wa Serikali TATU.


Hebu tujirejeshe kidogo kuitazama Nadharia ya Muungano.


Hoja za muudo wa serikali zinatafsiriwa na sababu kuu mbili ambazo ni hoja za kisheria na hasira za kisiasa.

1.HOJA ZA KISHERIA

Hoja za kisheria ni kwamba zinapoungana serikali mbili ni lazima pawepo na katiba ya serikali moja au tatu na wala sio mbili tena kisheria.Kwa mfano ni kwamba tume zote mbili zilizoundwa na Rais chini ya wasomi wa kisheria chini ya JAJI FRANSISI NYALALI na ile ya JAJI ROBERT KISANGA zote zilipendekeza serikali 3 na sio mbili.

Kwa mfano endapo utampa msomi wa kisheria kazi ya kukuandalia katiba ya serikali mbili zinazotakiwa kuungana atakuandalia katiba ya serikali ama 1 au 3 lakini sio mboli kwani hazipo kisheria.

2.HASIRA ZA KISIASA

Hasira za kisiasa ni sababu nyingine ya kuwa na serikali tatu,Kwa mfano mwaka 1984 aliyekuwa rais wa Zanzibar ABDU JUMBE aliasisi hoja ya kuwa na serikali 3 na ikamgharimu kunyang'anywa kadi ya CCM na kupoteza urais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na MZEE ALI HASAN MWINYI 1984-1985 kabla ya kuchukuliwa na IDRISA ABDUL WAKIL 1985-1990.

Mwaka 1993 paliibuka kundi la G55 liliokuwa na nia ya kuifufua Tanganyika kundi ambalo lilipelekea baraza la mawaziri kuvunjwa mwaka 1994 na baadhi ya mawaziri akiwemo waziri mkuu na makamu wa kwaza wa Rais kupoteza wadhifa wake.

Mwaka huo huo 1993 Zanzibar ilitaka kujiunga na OAC wakakataliwa kwamba hawana mamlaka ya kufanya hivyo ndipo aliyekuwa Rais wa wakati huo DR SALIMIN AMOUR JUMA akasema Zanzibar imedharauliwa na kuzidi kupandisha homa na hasira za Wazanzibar kudai mamlaka kamili ya Zanziabar.

Hata mwalimu Nyerere alikuwa na nia kwamba waunde serikali moja lakini kwa kuanzia alipendekeza kwamba waanze na serikali mbili ili wazanzibar wasiseme wamemezwa japo baadae alishindwa kuunda serikali moja.

Kwahiyo hizo ndio sababu za mkanganyiko uliopo Tanzania katika mchakato wa katiba mpya.

By Yericko Nyerere
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bado watanzania hawajaelewa hasa serikali tatu maana yake ni nn?

    ReplyDelete
  2. ujisemee wewe ucwasemee watanzania wengine wanaelewa na ndio maana wakazipendekeza hizo serikali tatu.

    ReplyDelete
  3. Watanzania wengi waliohojiwa hawakuongelea muundo wa serikali kama n tatzo. Ina maana watanzania wengi hawaoni serikali tatu kama ni suluhsho la matatzo yao, ila kuna masuala nyeti kama ya afya, elimu, uchumi n.k

    ReplyDelete
  4. serikali tatu au mbili hazina tija ila kinachotakiwa na jamii wapewe haki zao za msingi

    ReplyDelete

Top Post Ad