Karrueche Aomba Radhi Baada ya Kudiss Nywele za Mtoto wa Beyonce

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Karrueche Tran amewaomba radhi mashabiki wa Beyonce waliomshambulia kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudiss muonekano wa nywele za Blue Ivy kwenye tuzo za MTV VMAs, wakati akifanya kipindi cha 106& Park cha BET.

Karrueche aliponda muonekano wa nywele za Blue Ivy katika kipengele cha kipindi hicho kilichopewa jina la ‘Top 6 Things Blue Ivy thought about the VMA’s’, ambapo alisikika akisema kwa kumkariri Blue Ivy kuwa ‘Kweli niliamka hivi kwa sababu wazazi wangu hawakunichana nywele. Pole Blue! Nakupenda!”

Mashambulizi yaliyoendelea ndani ya siku mbili mfululizo yamemfanya mrembo huyo kuomba radhi kupitia Instagram akikiri kufanya makosa kwa kuwa yeye ni binadamu.

Katika maelezo yake, ameomba radhi kwa kutamka sentensi hiyo ambayo amesema ilitengenezwa kwenye muongozo wa kipindi na BET na ikapitia kwake.

BET wamewajibika pia na kueleza kuwa Karrueche alikuwa anasoma maelezo hayo kwenye teleprompter (screen ya kusomea habari kwenye TV) kama sehemu ya script na kwamba ilifanyiwa mabadiliko dakika kumi kabla ya kwenda hewani na hakupata nafasi ya kuipitia tena.

Huenda angekataa kuisoma kama angeipitia awali.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  2. huyu dada ana matatizo c bure

    ReplyDelete
  3. ndiyo rayaa ya watu wa nje wakingudua kuwa wapo wrong uwa ni wepesi wa kuomba msamaha ila ckibogo bogo ni watajaribu kukwepesha mada na kujitetea upande wao

    ReplyDelete

Top Post Ad