Raia wa Vietnam Akamatwa na Mzigo Mkubwa wa Meno ya Tembo na Kucha za Simba Uwanja wa Ndege Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi linamshikilia  Raia wa  Vietnam Dong Van(47) kwa kumkamata akiwa na meno 65 na kucha 447 za Simba kinyume cha sheria vyenye thamani ya Shilingi Milioni 189,420,000.

Kamishna Msaidizi  wa Polisi wa Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,  Hamisi Selemani, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana wakati alipotaka kusafirisha nyara hizo kwa kutumia Shirika la Ndege la Qatar Airways kwenda nchini Vietnam kupitia Doha.

Amesema alipopekuliwa alikutwa na nyara hizo ambazo alizihifadhi kwenye pakiti 7 za kahawa na pakiti moja ya mchele  na kuzichanganya na pakiti nyingine 15 za vyakula vya aina mbalimbali



Kamanda Selemani amesema  pakiti hizo ziliwekwa ndani ya begi la nguo ili kupoteza ushahidi wa aina ya mzigo alioubeba kwa wakaguzi wa uwanjani hapo.



Aidha amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania ni kichaka cha wahalifu,yaani hawatuogopi kabisa.
    tujiulize,ameweza vipi kufanya haya yote,kupita huko kote mpaka
    anaenda kushikiwa uwanja wa ndege?na sidhani kama hii ndio mara yake ya kwanza,
    ni dhahiri kuna mikono mingi ndio maana wanajiaminisha.shame on you Dong Van( DOG)

    ReplyDelete
    Replies
    1. DOG? Hahahahahahahahahahahahahahaha,mama mbavu zangu

      Delete
    2. no sio shame on Dong. shame on us. TZ... popote pale palipo legevu watu hufanya mambo kinyume. huyu sio kuchunguzwa ni kuhojiwa nani kamsaidia mpaka hapo na mnyororo wote uvutwe. huwezi kuondoa magugu pasipo kutoa mizizi yake. utakesha na shamba litakushinda. seriously tunacheza. hata samba nao??

      Delete
  2. ifikie stage tunyonge mmoja ili iwe fundisho kwa wengine .hao ni simba zaidi ya ishirini na tembo kazaa tunaenda wapi na tutafika kweli.kizazi kijacho kitakuwa hakini cha kurithi kwa namna hii.tusipokuwa makini na wenye hekima ,busara na utu vitu vyote vya asili vitatoweka .

    ReplyDelete
  3. MTUWEKEE NA SURA LABDA TUNAMJUA MAANA HUKU KWETU BAGAMOYO WAPO KIBAO

    ReplyDelete
  4. Ni kweli mdau mbona watanzania wakikamatwa na sembe nchi za watu wananyongwa! Ni vyema na wao wanyongweeee tuwaonyeshe mfano!

    ReplyDelete
  5. huyo ni jini mufilisi! tukiwachekea tu tujue kabisa mbuga zetu zitabakiwa na NUNGUNUNGU peke yao! swala la huruma liondolewe hapo!

    ReplyDelete
  6. kwa nini serikali isianzishe sharia ya kunyonga kwa yeyote atakae kamatwa na nyaraka za taifa?

    ReplyDelete

Top Post Ad