Baada ya kutemana na Edzen, Dida Amtambulisha Mchumba Wake Mpya Siku ya Birthday yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SIKU chache baada ya kudai hawezi kuolewa kwa sasa, mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’, ameonesha matumaini mapya ya kuolewa baada ya kumwanika mchumba’ke mpya.

Dalili za matumaini hayo mapya zilionekana usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita katika sherehe yake ya kuzaliwa (bethidei) iliyofanyaka nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao Bongo.

Miongoni mwa wasanii waliohudhuria hafla hiyo ya kufuru ni pamoja na malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa na waigizaji; Chuchu Hans, Jacob Steven ‘JB’, Rose Ndauka, Salma Salmin ‘Sandra’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Jeniffer Kyaka ‘Odama’, Maimatha Jese na wengine kibao ambao walimpa Dida kampani ya nguvu na kumtunza fedha na zawadi mbalimbali.



Kama hiyo haitoshi, kwenye hafla hiyo, kulitawaliwa na vinywaji vya kila aina huku kukiwa akichinja mbuzi watatu maalum kwa ajili ya sherehe hiyo sambamba na kuku kibao wa kienyeji, nyama za kila aina, msosi wa nguvu na pombe za kumwaga

Wakati sherehe ikiendelea, Dida aliibua minong’ono ya aina yake baada ya kutambulisha uwepo wa shemeji zake waliotoka Arusha ambao walimwakilisha mchumba wake katika pati hiyo.
“Jamani humu ndani kuna watu mbalimbali ambao wamefika kuniunga mkono, mkiwemo wasanii wanahabari pamoja na watangazaji wenzangu, lakini kikubwa zaidi napenda kutambua uwepo wa shemeji zangu waliofunga safari kutoka Arusha, wamekuja kuniunga mkono, nimefurahi sana,” alisikika Dida.

Ulipofika muda wa kutoa zawadi, mmoja wa mashemeji zake hao aliyejitambulisha kwa jina la Feisal alishika kipaza sauti na kusema alitinga kwenye hafla hiyo kumwakilisha ndugu yake (jina alilihifadhi) ambaye alimtuma amwambie Dida kuwa amemzawadia gari lenye thamani ya Sh. milioni 26 za madafu ambalo siku si nyingi litatua Dar.

“Hehee my new baby, huyo ndiye my new baby jamani na hawa ndiyo mashemeji zangu wa ukweli,” alipaza sauti Dida.


Alipoulizwa na mwandishi wetu juu ya mipango yake na mchumba huyo mpya, Dida alifunguka:
“Huyo ndiye mwanaume wangu wa sasa muda ukiwadia nitaanika kila kitu, bado mapema mno kuzungumza mengi,” alisema Dida ambaye kama ataolewa na mwanaume huyo itakuwa ndoa ya nne.

Dida aliyemwagana na Ezden Jumanne miezi kadhaa iliyopita, kabla ya hapo aliwahi kuolewa na wanaume wawili tofauti ambao alimwagana nao kwa talaka.

Waandishi: Mayasa Mariwata, Musa Mateja na Imelda Mtema

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ehe ehe eheeeeeeeeeee! amakweli kuna wanaume hawana kinyaa, hilo GUBEGUBE limechumbiwa!!? yetu macho na masikio, kwani kuolewa si'kazi kazi ni kuilea ndoa!

    ReplyDelete
  2. Waiii wache wenye mapene Yao watawale mapenzi.komaa hivyohivyo dida.kunya anye kuku akinya bata kahara mumuache dida aishi atakavyo

    ReplyDelete
  3. Halwa haina makombooooo

    ReplyDelete

Top Post Ad