Ray C Aifuta Kesi ya Mwanamuziki Chid Benz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakati nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na madawa ya kulevya akiwa njiani kuelekea Mbeya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyekuwa amemfungulia kesi ya kumpiga katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, amefuta shauri hilo na kumsamehe.

Akiongea na Gpl, Ray C alisema ameamua kumsamehe kwa sababu yeye ni mtu wa Mungu na anaamini yanayomtokea ni ishara ya kumtambulisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya hayafai.

“Mimi ni mtu wa Mungu, nimemsamehe na wala sitaki kesi naye, lakini kumsamehe mimi peke yangu hakusaidii, Watanzania wote kwa pamoja tumuombee ili jambo hili limalizike na likiisha, ninamuomba aje tushiriki pamoja katika tiba ya Methadone,” alisema.

Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika waraka katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana na matumizi hayo ya madawa ya kulevya.

“Pole kaka yangu Chid Benz, naumia kuona tatizo ulilokuwa nalo bado haujalitafutia jibu, mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi pamoja. Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu,” yalisomeka baadhi ya maandishi yake mtandaoni.

Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo cha kukamatwa kwake na madawa hayo kitakuwa ni jibu zuri kwake kuwa anakoenda si salama na kumtaka abadili njia na kuungana naye kwenye tiba ya Methadone kwani ndiyo kiboko ya madawa ya kulevya.

Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za madawa ya kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad