Mabomu Yatawala Mbagala katika Maandamano ya CUF.....Profesa Lipumba na Wafuasi wake Watiwa Mbaroni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho,Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.


Awali polisi ilizuia  maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya  kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara yalifanywa na vyombo vya usalama.


Akizungumza leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro alisema wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati ya hao wawili ni wanawake na 30 ni wanaume ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.

“Wanachama 32 akiwemo Profesa Lipumba tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati kwa kufanya maandamano ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea kuwahoji,”alisema Siro.

Siro alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo na viongozi wa chama hicho hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.

Siro alisema sababu kubwa ya kuzuia maandamano hayo yasifanyike kwa kuwa mwaka 2001 yalifanyika maandamano batili yaliyosababisha baadhi ya polisi na wananchi kufa.

“Jeshi la polisi likiruhusu hayo maandamano kuna uwezekano wa kutokea fujo na hayo maandamano ya mwaka 2001 yalikuwa si halali na kwenye maandamano hayo walikufa askari polisi,”alisema Siro.

Alisema sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo ni kuwa hivi karibuni walikamatwa watu wanaojihusisha na mambo ya ugaidi hivyo kutokana na mazingira hayo jeshi la polisi linazuia mikusanyiko mikubwa kwa kuhofia kutokea mambo mabaya.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad