Auawa na Wananchi kwa Kupeleka Waganga Kijijini Kilimanjaro Kwa Ajili ya Kusindika Nyumba yake na Kupiga Ramli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MZEE mwenye umri wa miaka 68, Celestine Mushi, mkazi wa kata ya Motamburu wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, ameuawa na wananchi wanaotajwa kukasirishwa na kitendo chake cha kupeleka waganga wa jadi kijijini kwa lengo la kuifanyia zindiko nyumba yake.

Mushi anadaiwa kuwatoa waganga hao wawili jijini Dar es Salaam na kuwapeleka Rombo kwa kazi hiyo maalumu.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kamwela aliyesema mauaji hayo yalitokea juzi saa 2.30 usiku nyumbani kwa Mushi katika kitongoji cha Mbomai Juu, wakati waganga hao wakiendelea na zindiko lao.

Kamwela aliwataja wanaodhaniwa ni waganga wa jadi kuwa ni Ashraf Mjengwa (22) na Peter Mmaka (25), wote wakazi wa Magomeni, Dar es Salaam.

Alisema waganga hao walifika nyumbani kwa Mushi juzi saa 10 jioni, na ilipofika saa 11 walianza shughuli ya zindiko na walipomaliza, Mushi alitaka kuwapeleka katika nyumba ya mkwe wake aitwaye Priscila Hilment, ili nayo ifanyiwe zindiko.

Kamwela alisema kitendo hicho kilikataliwa na mama mkwe, ambaye alipiga kelele kuomba msaada kwa wananchi ili wawaondoe waganga hao, ambapo wananchi walifika na kuwashambulia waganga hao.

Alisema kutokana na tafrani hiyo, raia mmoja alitoa taarifa katika kituo cha polisi, ambapo polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumwokoa mganga mmoja, Mjengwa, ambapo mwenzake alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Kamwela alisema ilipofika saa 2 usiku, kundi la wananchi wasiojulikana idadi yake walirudi nyumbani kwa mzee huyo na kuanza kumpiga kwa fimbo kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake, na kisha kuondoka na kumwacha akivuja damu nyingi.

Alisema kutokana na damu kuendelea kuvuja, mtoto wa mzee huyo alimchukua baba yake na kumpeleka katika kituo cha afya cha Tarakea, ambapo alifariki dunia kabla ya kupatiwa matibabu na Jeshi la Polisi limeanza msako wa kuwatafuta wahusika.

Mwanajeshi ajinyonga Wakati hayo yakitokea mkoani Kilimanjaro, Grace Chilongola anaripoti kutoka Mwanza kuwa, fundi wa magari wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi namba 512 MTC Nyegezi, jijini Mwanza, Jacob Mponeja (55) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani huku akiacha ujumbe.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Joseph Lusungu tukio hilo lilitokea Aprili mosi mwaka huu majira ya saa moja asubuhi.

Alisema ujumbe huo ulioandikwa kwenye kitabu kidogo kilichokutwa kwenye eneo la tukio ulisomeka; “Kifo changu kimetokana na mke wangu kujihusisha na vitendo vya kishirikina, hali iliyosababisha kutaka kuuawa mara mbili na mtu asilaumiwe kwa kifo changu.”

Alisema kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, ambaye ni mwanafunzi katika sekondari ya Nyabulogoya, kabla ya tukio la kujinyonga, baba na mama yake Happy Mabula (45), walikuwa na ugomvi mkubwa.

Kaimu Kamanda huyo alisema katika ugomvi huo mama huyo alikatwa shoka na mumewe na kwamba alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu na kwamba hali yake sio nzuri.

Alisema katika eneo la tukio kulikutwa shoka lililokuwa na damu pamoja na kitabu hicho kidogo kilichokuwa na ujumbe ulioandikwa na marehemu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad