Kajala Awaongoza Mastaa Kumtuliza Wema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia kauli ya Wema Sepetu ya hivi karibuni kuwa hawezi kupata mtoto wa kumzaa, mastaa wa fani mbalimbali wamejitokeza kumtuliza moyo, wakiongozwa na hasimu wake wa karibu, Kajala Masanja, ambaye amesema hana sababu ya kukata tamaa, kwani bado ni mdogo.

Akizungumza na na gazeti la Risasi Mchanganyiko baada ya kuombwa maoni yake, Kajala alielezea masikitiko yake juu ya hali ya rafiki yake wa zamani, lakini akasema anaamini hana tatizo kubwa la kumfanya asipate kabisa mtoto, isipokuwa anadhani bado hayampata mtaalamu sahihi wa masuala ya wanawake anayeweza kumsaidia tatizo alilonalo.

“Namuombea sana kwa Mungu, lakini sitaki kabisa kuamini kama hawezi kupata mtoto katika maisha yake, mbona bado kijana sana, atapata tu bwana,” alisema Kajala, ambaye ana mtoto aitwaye Paula.“Sitaki kuamini,  roho inaniuma sana, namshauri Wema asiumie wala kuwa mnyonge. Na watu waache kumuumiza kwa maneno ya kebehi, lakini kama Wema akiwa tayari kulea mtoto wa mwenzake, anione, nina imani atapata mtoto atamlea na kumtunza kama wake.

“Naomba achukue mfano wangu mimi Wastara, Mungu kanipokonya mguu kanipa watoto, natumia mguu wa bandia na ninatembea lakini Wema amepewa kila kitu kasoro mtoto, atumie mtoto ambaye siyo wa kumzaa amlee kama wa kwake na hapo machungu, huzuni na mawazo vitaisha na atamzoa kama wa kwake,” alisema Wastara Juma.

Wengine waliompa pole na kumtakia nguvu kukabiliana na tatizo lake ni pamoja na Jini Kabula, Salome Urassa ‘Thea’, Aisha Bui, Amanda Posh na Baby Madaha ambaye alisema;

“Mtoto siyo mwisho wa maisha, kuna mastaa wengi tu ambao hawana watoto na wanaishi kwa amani kama Oprah, Tyra Banks na wengineo, hivyo siyo ishu kubwa kihivyo, watu waache kumsakama Wema, mimi mwenyewe sina mpango wa kuwa na mtoto.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani kafiwa jamani?

    ReplyDelete
  2. Aolewe kwanza labda katika ndoa mungu atambariki in sha Allah,

    ReplyDelete
    Replies
    1. WEWE UMESEMA. WEMA OLEWA KWANZA NDO UJUE KAMA UNA UWEZO WA KUZAA AU LAA.PENGINE NI UTULIVU TU UNAHITAJI NA KUWA NA MUME WATU TUMETOFAUTIANA. MUNGU NI MWEMA UTAPATA TU MTOTO AMINI HIVYO.

      Delete
  3. Tatizo anataka kupata mtoto nje ya ndoa, huo sio Mpango wa Mungu. Mpango wa Mungu pamoja na mila na desturi zetu waafrika mtu anatakiwa aolewe ndio azae lakini mastaa wanajifanya hawajui hilo wanataka kuzaa bila hata ndoa.

    ReplyDelete
  4. WEMA NAYEEE. FUATA MAEREKEZO! KAMA JAY MILION UTAPATA TULIA

    ReplyDelete
  5. Kwanza Bora hakuzaa na x boyfriend wake kwa sababu walikuwa hawamechi because she is so pretty. Nina imani atazaa

    ReplyDelete
  6. baby Madaha are you serious?

    ReplyDelete
  7. BABBY MADAHA TENGUA KAULI YAKO PLZ ,,,,,,,,,,,MAANDIKO YANASEMAULIMI NDIKO KULIKO UZIMA NA MAUTI SHAURI YAKO

    ReplyDelete

Top Post Ad