Mrembo Mtanzania Afia China Baada ya Kuugua Kwa Muda Mrefu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mrembo Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Rehema Mohamed (30), anadaiwa kufia katika Mji wa Shanghai nchini China wiki mbili zilizopita baada ya kuugua kwa muda mrefu hadi mauti yalipomfika huku ndugu zake wakichanganyikiwa kutokana na taarifa za kifo hicho.

Habari zaidi kutoka kwa aliyekuwa rafiki wa karibu wa Rehema nchini China, (jina lake linahifadhiwa) zinasema kuwa wamekuwa wakihangaika ili kupata fedha za kusafirisha mwili huo lakini imekuwa ngumu kupatikana.

Chanzo hicho kilisema kuwa kimefanya mawasiliano na baadhi ya ndugu wa marehemu ambao nao wanajikusanya kwa ajili ya kupata fedha hizo ili kuurudisha mwili nyumbani Dar kwa mazishi.

“Yaani huku tunapata tabu sana na tuna uchungu kwa kuwa fedha zilikuwa zikihitajika nyingi sana lakini tunashukuru taratibu zinaenda sawa karibu tutaleta mwili nyumbani,” alisema rafiki huyo.

Mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema kuwa kifo cha ndugu yao ni pigo kubwa ukizingatia amefia ughaibuni na fedha za kumleta zinahitajika nyingi hivyo wamekaa na kumuomba Mungu ili mwili ufike Bongo waupumzishe.

“Msiba wa mdogo wetu umetupa wakati mgumu sana jamani, ukizingatia amefia mbali sana na kumleta huku ni fedha nyingi mno, hivyo tunamuomba Mungu tu ili mwili ufike na tuupumzishe katika makaburi ya nyumbani,” alisema ndugu huyo.

Toa Maoni Yako Hapa Chini
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sijaona mashiko ya habari hii!!!!!mtu yoyote akifa ndugu na marafiki lazima wawe na uchungu,au ukosefu wa fedha ya kusafirisha mwili ndio habari?wekeni habari zenye kueleweka

    ReplyDelete
  2. innalillah wainna ilayhi raj..uuun

    ReplyDelete
  3. Alienda kufanya shughuli gani huko maana watu wanaenda huko but hawana cha maana kilichowapeleka.
    anyway poleni wafiwa

    ReplyDelete
  4. Alienda huko kufanya shughuli gani?maana wabongo tunakimbilia nje bila shughuli maalumu zaidi tu ya kuuza sura.
    anyway poleni wafiwa

    ReplyDelete
  5. Tatizo wabongo wengi tunapenda kukimbilia nje hata kama hatuna shughuli ya maana ya kutupeleka huko.Yanapotokea matatizo kama haya watu wanaanza kuhaha kusafirisha mwili.,poleni wafiwa

    ReplyDelete

Top Post Ad