Sakata la Emmanuel Mbasha Kubaka: Daktari Atoa Ushahidi Mahakamani, Asema Vipimo Havikuonyesha Dalili yoyote ya Msichana Huyo Kubakwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shahidi wa nne katika kesi ya tuhuma za ubakaji inayomkabili Emmanuel Mbasha, mume wa mwanamuziki wa nyimbo za injili, Flora Mbasha, jana alidai mahakamani kuwa hakuona dalili zozote za kuingiliwa kimwili mlalamikaji.

Hayo yalidaiwa na daktari wa Hospitali ya Amana, Migole Mtuka, ambaye alimfanyia vipimo msichana huyo.

Daktari huyo alidai katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwamba vipimo alivyomfanyia msichana huyo anayedaiwa kubakwa na Mbasha, havikuonyesha kitu chochote.

Dk. Migole alidai kuwa binti huyo alifika hospitalini hapo Mei 26, mwaka jana, kwa alili ya kufanyiwa vipimo.

Alidai kwamba binti huyo alipofika hospitalini hapo, alimfanyia kwanza vipimo vya macho kisha kumtaka kwenda kufanya vipimo vya maabara, ambavyo hutolewa bure.

Dk. Migole  alidai kwamba baada ya kumtaka kwenda kufanya vipimo vya maabara, akiwa na baadhi ya ndugu wa familia yake, hakwenda bali aliingia mitini na kurejea Juni 3, mwaka jana, baada siku nane kupita.

Alidai baada ya kufanyiwa hivyo, vipimo hivyo  vilionyesha kuwa hakuna kitu chochote alichofanyiwa, kwa maana ya kubakwa au kuingiliwa na mwanamume katika mwili wake na kuwajazia fomu aina ya PF3 kwa kile alichokiona.

Binti huyo hakuonekana kuwa na ujauzito, maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na wala mbegu za kiume katika sehemu za siri,” alidai daktari huyo.

Hata hivyo, baada ya kutolewa ushahidi huo, Hakimu Flora  Mujaya, hawakuweza kusikiliza ushahidi mwingine kutokana na taarifa za msiba wa hakimu mwenzao, zilizofika mahakamani hapo.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa upande wa Jamhuri Aprili 20, mwaka huu.

Mbasha anadaiwa kuwa Mei 23 na 25, mwaka jana, alimbaka binti  mwenye umri wa miaka 17, ambaye anadaiwa ni shemeji yake  huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. FLORA UMEUMBUKA

    ReplyDelete
  2. Inabidi abadilishiwe kipande yeye Flora an ajibu mashtaka ya kumsingizia mumewe na kumuibia mali zake. Malaya huyu na mdogo wake

    ReplyDelete
  3. HIVI SIKU NANE BAADA YA KUBAKWA ANGEWEZA KUONA MBEGU ZA KIUME KWENYE UKE?ALIKUWA HANAWI WALA KWENDA HAJA NDOGO?SIJUI !

    ReplyDelete
    Replies
    1. KWANINI ALIKIMBIA SIKU AMBAYO ALITAKIWA KUFANYIWA VIPIMO??? HAKUNA CHA KUBAKWA HAPO WALA NINI!! HAO NDUGU ZAKE KWANINI WALIONDOKA NAYE BILA VIPIMO NA WAKATI WALIAMBIWA WAENDE MAHABARA KUPIMA???????? NADHANI HAO NDUGU ZAKE NI WATU WAZIMA WANAELEWA FIKA NINI WANAMFANYIA EMMANUEL.
      MUNGU ATAWAUMBUA.

      Delete
  4. Kumbuka kuwa siku aliyotakiwa kufanyiwa vipimo aliingia mitini kwa hiyo kama alitendewa uovu huo kwanini alikimbia ???

    ReplyDelete

Top Post Ad