Zitto Kabwe Aipasua Ngome Ya CHADEMA Jijini Mwanza......Melfu ya Wananchi Wafurika Viwanja vya Furahisha Kumsikiliza, Juhudi za CHADEMA Kuvuruga Mkutano Zakwama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Juhudi  za  Chama  cha  Demokrasia  na  Maendeleo  kuuvuruga  mkutano  wa  ACT -Wazalendo  jana  ziligonga  mwamba  baada  ya  Maelfu  ya  wananchi  kufurika  katika  viwanja  vya  Furahisha  kuwasikiliza  viongozi  wa  chama  hicho  huku  ulinzi  ukiwa  umeimarishwa  katika  kila  kona  ya  uwanja  huo.

Mpekuzi  ilishuhudia  Difenda  tatu  za  polisi zikifanya  doria  katika  uwanja  huo  huku  polisi  wakiwa  tayari  kwa  lolote.

Ulinzi  uliimarishwa  katika  viwanja  hivyo  kutokana  na  kauli  ya Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, John Mnyika  aliyoitoa  juzi  katika  viwanja  hivyo  ikiwa  ni  siku  moja  tu  kabla  ya  mkutano  wa  ACT-Wazalendo  kufanyika.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi ambao  ulihudhuriwa  na  wafuasi  wachache  wa  chama  hicho, Mnyika alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao’.

Katika  hotuba  yake, huku  akinukuu  baadhi  ya  vifungu  vya  biblia  na  Quruan, Mnyika  aliwataka  wafuasi  na  wapenzi  wa  CHADEMA  kumkabili  Zitto  Kabwe  kwa  namna  yoyote  kwa  kuwa  ni  adui  wa  chama  chao  na  ujio  wake  jijini  Mwanza ulikuwa  na  lengo  la  kukiharibu  chama  chao..
 
“Mtume Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili na sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono Ukawa halafu mnawakaribisha?
 
Nendeni kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto. Sikilizeni niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana kuanzia EPA mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni aliyasema haya kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki Ukawa,” alisema Mnyika.
   
Zitto Kabwe  Ajibu  Mapigo
Akihutubia mamia ya wananchi wa Mwanza jana, Zitto alisema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha.
 
Zitto alisema pamoja na hali hiyo, ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya njema kwa siasa za upinzani.
 
Alisema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele.
 
“Mwanzo walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo likafanyika, tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili ya kugawa upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa ajili ya kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu kutambua watu gani hawataki kuiondoa CCM,” alisema Zitto.
 
Alisema wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.
 
“Sisi ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi. Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi,” alisema na kuongeza:
 
“Sikufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana…mmoja kwa kukosa busara na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni na kutoa siri za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.
 
“Tunakuja na jahazi jipya ambalo ndugu zangu wa Mwanza nimekuja kuwakabidhi, kubwa tunataka kulirudisha taifa katika misingi yake ya ujamaa na kujitegemea, tunahitaji ujamaa wa demokrasia,” alisema Zitto.
 
Alisema tafsiri ya ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali za watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.

 
Apata Mapokezi  ya  Kutisha:
Zitto ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira, waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata mapokezi makubwa yaliyoanzia wilayani Misungwi.

Alipofika  katikati  ya  jiji  la  Mwanza, Maelfu  ya  wananchi  waliuzia  msafara  huo  na  kuanza  kulisukuma  Gari  la  Zitto.

Hali  hiyo  ilisababisha  foleni  kubwa  ambapo  trafiki  waliingilia  kati  na  kumtaka  Zitto  Awashe  gari  kunusuru  Foleni.
 
Safari  ya  kulekea  Viwanja  vya  Furahisha iliendelea  ambapo mapokezi hayo yakiongozwa na vijana waendesha pikipiki (bodaboda) na kikundi cha wanawake yaliusindikiza  msafaa  huo  hadi ulipoingia kwenye uwanja wa Furahisha.
 Leo  ni  zamu  ya  Musoma:
ACT- Wazalendo  leo  wanatarajia  kufanya  mkutano  wa  hadhara  Musoma. 
  
Habari  tulizozipata  zinadai  kuwa baada  ya  CHADEMA  Kuvuruga  jijini  Mwanza  juzi, jana  walikuwa  Musoma  ambapo  kauli  yao  ilikuwa  ni  ileile  ya  kuwataka  wananchi  kutohudhiria  mikutano  ya  Zitto  Kabwe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Boooo,si wote tulioenda na wafuasi wa zitto wengine tulienda kumchora tu.

    ReplyDelete
  2. Chadema your just a small

    ReplyDelete
  3. huyo mnyika nataka zito aje kugombea ubunge ubungo tuone kama hajatafuta pa kujificha..nawashangaa wapinzani kama huyo slaa ooh epa sijui nini WE WANT THE WAY FOWARD...HAPO CHADEMA VISION HIYO HAKUNA

    ReplyDelete
  4. sio wote tuliokuwa hapo ni act

    ReplyDelete
    Replies
    1. No matter what, kama ulihudhulia basi ujue si yote yaliyoongelewa mkutanoni yalikuponyoka. Bali I believe yapo yaliyonasa akilini mwako

      Delete
  5. CHADEMA MNAONESHA SIASA GANI MBONA MNAJIAIBISHA HEBU JIPANGENI NA SERA MADHUBUTI KWA AJILI YA UCHAGUZI UNAOKUJA SIO MGOMBANE ZITO

    ReplyDelete

Top Post Ad