Adam Juma 'Hanscana na Nisher ' Watakuua Kwa Pressure'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Juzi kupitia ukurasa wake wa Instagram Director Mkongwe Adam Juma aliweka post ambayo ni wazi alionyesha kukerwa na mambo mbalimbali ambayo yanaendelea katika tasnia ya filamu na muziki kiujumla, ambapo kwa tafsiri
ya haraka haraka Adam anaonyesha wazi kuwa kuna watu ambao wapo muda mfupi katika tasnia hiyo na kujiona kama wamemaliza kila jambo wakati yeye ni mkongwe ila anazidi kuijifunza kila siku, jambo ambalo anaamini litamfanya aendelee kuwepo siku zote ukilinganisha na watu ambao wameridhika na mafanikio ya muda mfupi na kujisahau na kudai kuwa kamwe hawatatoka.

"Watanzania wabishi sana, miaka mitatu tu mtu anaanza kujifanya anajua kumpita mungu,,, kwa style hii hakuna atakae toka i swear to god!!!! Mimi kila siku najifunza ili siku moja nifanye kazi ninayoipenda kwa umakini sio kutengeneza video tu!!!! Wengine wanaona kushika kamera na kushot ndio mwisho, tunafanya kazi na watu wengine njee tunajifunza sana vitu mkiona nimenyamaza mnaona kama mimi fala vile, ngoja sasa.

Baada ya kutoa kauli ambayo kwa mashabiki wameipokea kama Adam amepaniki kutokana na ukali wa maneno ambayo alitumia kufikisha ujumbe huo, baada ya kuweka ujumbe wake huo katika Ukurasa wa Facebook wa East Africa Radio/ www.facebook.com/EARadio mashabiki walitoa maneno yao kwa Adam ikiwa pamoja na kumshauri kuwa yeye ni mtu mzima anaweza kufikisha ujumbe kwa namna nzuri pasipo kutoa makwazo kwa watu kutokana na heshima ambayo tayari kajijengea nyuma kwa kufanya kazi nzuri na kuleta changamoto na uboreshaji katika tasnia hiyo kwa miaka kadhaa huko nyuma.

Adorn Leonidas nadhani ni hasira tu, mtu akiwa na hasira anaweza kuongea chochote. Namshauri aturie tu atawatukana wangapi?
Lakini baadhi ya mashabiki wao wanaamini kuwa huenda maneno yaliyomtoka Adam Juma ni kwa sababu ya changamoto anayoipata kutoka kwa waongozaji wadogo katika tasnia hiyo ambao kwa sasa wanafanya vizuri, na kufunguka mambo mengi kutokana na ushindani wao wenyewe na hapa ndipo mashabiki hao walipoamini kuwa vijana hao wanampa sana Changamoto Adam na kuandika haya.

"Michael Dilunga Hanscana na Nisher watakupa presha broo fanya kazi, Ronaldinho alikuwa anaupiga mpira mwingi sana lakini sasa hivi kafunikwa na kina Messi. wanaokulewa watakuelewa tuu siku zote fanya kazi mkubwa achana na maneno kama hayo

"Riziki Rajab Hanscana anawaumiza kichwa kama Kiba vile huku upande wa pili"

"Ebbyno Chiboko ujuwe nini ..! Mtu anae karibiwa na kifo utamjuwa tu..uropokaropoka tu hovyo...
Kama kuna alie mzinguwa nae aende kimyakimya tu akamzinguwe..kutafuta mashahidi hiyo ni kesi."

"Prince Hans Maxwell Huyo muoga tuu hana lolote kama haogopi kwanini asimtaje, mbona 2Pac alimchana makavu Big, F..k Big, F..k Bad boys, F..CK Mob deep na akamalizia if u are down with bad boys F..ck u too.

Shafii Mahmoud usibishane na kuamua kuchimba biti, piga kazi bhana maneno ya nini Adam!
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad