Edward Lowassa Aongea na Vyombo vya Habari LEO....... Adai hahusiki na Kashfa ya Richmond, Hana Mpango wa Kuhama CCM na Yupo Tayari Kupima Afya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu mstaafu  Edward Lowassa leo amefanya  mkutano maalum nyumbani kwake mjini Dodoma  na  wahariri  wakuu  wa  vyomba  mbalimbali  vya  habari  hapa  nchini. Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo;

1. Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji.

 Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta.

Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii.(Jumamosi)

2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo .

Pia aliyekuwa mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeti Misoki ametangazwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano katika timu ya kampeni ya Lowassa. Amehoji kwani akina Karamagi wana tatizo gani na kwani wao sio binadamu?

3. Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo kwanza . Amesema serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza.

4. Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na ataendelea kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake na haina madhara yotote.

5. Anasema hatahama CCM na asiyemtaka yeye CCM ndie aondoke ndani ya chama kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi kuwania urais.

6. Amesema hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa. Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu.

7. Amesema Arusha itawaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.

Bonyeza Hapa Kumsikiliza:

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Baba hongera uko makini sana,una vision,na ujasiri wa kweli ukoa nchi,yetu imekuwa kama shamba la babu kila mtu anachuma na kukimbia,ulinzi wa nchi,elimu,afya uvipe nafasi ya kwanza,sio majambazi yanafunga mtaa.

    ReplyDelete
  2. big up to him!! ukawa kaeni chonjo simba kakasirika msituni! a person that can make hard decision, he is well determined and he can make changes.

    ReplyDelete

Top Post Ad