JE Thamani ya Yamoto Band ni Nyumba na Gari ?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Saidi fella ni mfanyabiashara Katika tasnia ya Muziki na mafanikio ya hii band kwa asilimia zote yeye ndio kayawezesha. Kwa hili nampa Hongera sana

Kilichonifanya niandike huu uzi ni Tukio ambalo limetokea jana ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya kiongozi wa band hiyo Aslay, katika siku hiyo ndugu Fella alitoa zawadi ya gari dogo kwa kijana wake. Sambamba na hili Fella ameshatangazia uma kuwa Nyumba za hawa vijana watakabidhiwa mwezi wa saba na pengine Rais akawa mgeni rasmi. Nimpongeze tena Fella kwa hatua hii nzuri

Ninachojiuliza hapa na kilichopelekea kuandika huu uzi ni Je nini thamani ya mziki wa hawa vijana? Mimi sio mtaalam wa kutathimini mziki ila kitu kimoja ambacho nina uhakika ni kuwa hawa vijana wana kipaji kikubwa chenye thamani zaidi ya hili gari na hizo Nyumba watakazopewa. Najua utajiuliza iweje niseme hivi Wakati hizo Nyumba sijaziona, naongea haya kwa uzoefu wa Fella kwani amekuwa akiwanunulia Nyumba wasanii wake Temba na Chege,

Mara ya mwisho nilimuona Fella akimkabidhi Temba Nyumba aliyomnunulia nje ya mji. Kimsingi ile Nyumba ilikuwa ni ya kawaida sana na ni Nyumba ambayo ilikuwa chakavu kwa kiasi fulani. Thamani ya Temba na Chege Sidhani kama ni sawa na Nyumba ya namna ile. Kutokana na hilo ndio maana naamini hata hawa vijana wa Yamoto nao watapewa Nyumba za ubora wa kawaida ambayo si linganifu na thamani ya vipaji vyao.

Kwanini Fella uwanunulie Au kuwajengea Nyumba wasanii wako? Kwanini usiwape hela zao wafanye yao wewe ubaki kuwasimamia na kuwakumbusha umuhimu wa kufanya maendeleo. Wasanii wako sio Watoto kiasi kwamba washindwe kusimamia ujenzi Au ununuzi wa Nyumba zao. Kitendo hiki cha kuwajengea Au kuwanunulia Nyumba kinaficha Mengi juu ya gharama halisi za manunuzi.

Mbona dimond Nyumba yake hamjamjengea Au kumnunulia? Hili ni swali ambalo nawaachia Yamoto band,Chege na Temba. Ifike mahali msanii awe mwajiri wa manager na sio kinyume chake, ndio maana Diamond anafanikiwa sababu yeye kawaajiri Fela na Babu Tale japo mbele ya Jamii huwa anajishusha ili ionekane kama Hao wawili ni maboss zake

By xfactor
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wasanii amkeni,, hawa jamaa wanawanyonya vibaya mno

    ReplyDelete
  2. Wanawatumia madogo, wenyewe bila kujijua, wao wanaendelea kupiga chapaaa ndefuuu dogo wanawaminyia, wakati ndio huu, madogo hamkeni, msingoje kesho

    ReplyDelete
  3. Wewe unayeona nimewapa chini ya uwezo wao umewasaidia nini hawa vijana kama si kudowload nyimbo zao ktk pc na kuzitumia bure?
    Watanzania acheni ushamba kwani wasanii wangapi wanasota muaka nenda rudi na hawana hata baiskeli?Mimi kuwathamini vijana wangu wewe unachukua,wivu wa kininga huo!

    ReplyDelete
  4. basi wamlipe ada za shule walizokuwa wanalipiwa na chakula walichokula miaka hii yote,na nguo walizokuwa wanavaa miaka yote hiyo na matibabu walipewa.halafu hao ni watoto tu waacheni na baba yao.msije mkawavimbisha kichwa wakaanza ugomvi kama Dongo Janja

    ReplyDelete
  5. Msisahau hizi ni zama za kibepari, mambo haya hayatakwepeka kamwe.

    ReplyDelete
  6. Msisahau kuwa hizi ni zama za kibepari, mambo ya namna hii hayakwepeki.

    ReplyDelete

Top Post Ad