Mume wa Zari Ivan Anaswa Kwa Shosti wa Zari Ambaye ni Model Maarufu Uganda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kampala, Uganda
Habari kutoka nyumba ya jirani nchini Uganda ikufikie kwamba aliyekuwa mume wa mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, tajiri Ivan Ssemwanga anadaiwa kunasa penzi la shosti wa kufa na kuzikana wa mkewe huyo aitwaye Stella Nankya, Ijumaa Wikienda limetonywa.

Ubuyu kutoka jijini Kampala nchini humo ulidadavua kwamba, Ivan na Stella ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’, hivi karibuni wamekuwa wakijiachia kimalovee kwa raha zao.

Tukio la juzikati lililoacha gumzo ni pale wawili hao waliponaswa wakiwa wamegandana kimahaba kwenye Ukumbi wa Ekitone uliopo Pretoria nchini Afrika Kusini ambapo kulikuwa na tamasha la muziki.

“Walikaa pamoja, walijiachia pamoja ziro ‘distansi’ kwani hakukuwa na kitu cha kuwatenganisha kati yao. Kwa kweli walionekana ‘kapo’ ya kupendeza mno,” alisema shuhuda wa tukio hilo na kukaririwa na gazeti moja la nchini Uganda.

Kufuatia urafiki wa Stella na Zari walivyokuwa wameshibana, mashabiki wao wamekuwa na maoni tofauti huku Stella akionekana msaliti kwa Zari.

Habari nyingine zilidai kwamba, Ivan ameamua kufanya hivyo ikiwa kama kisasi au kumrusha roho Zari aliyezaa naye watoto watatu ambapo anatarajia kumzalia Diamond siku chache zijazo.

Ilielezwa kuwa, Stella alipoulizwa kwa nini ameamua kumsaliti rafiki yake Zari kwa kutembea na Ivan alisema kwa kifupi:

“Sitaki kuwa karibu na mtu mkavu (Zari), na mimi nimeamua kuwa mkavu.”

Zari au mama kijacho na Stella walikuwa ni marafiki wakubwa ambapo kuna wakati Zari alimpa sapoti ya nguvu Stella alipokwenda kuiwakilisha Uganda kwenye mashindano ya urembo ya Miss Asia Pacific huko Seoul nchini Korea Kusini ambapo walisafiri wote.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie nao matako kweli sasa hii habari ya nini waache wapigane miti tatizo ni nini kwani

    ReplyDelete
  2. Hii sasa iko pouwa tena imekaa vizuri. Wewe ukisema CHANINI wenzio wanajiuliza NITAKIPATA LINI!

    ReplyDelete
  3. Duuuh! inauma hiyo.............................!!!!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad