Padri wa Kanisa Katoliki Anaswa Kichakani Ndani Ya Gari Akiwa Na Mrembo UCHI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KAMA mti mbichi unatenda haya, itakuwaje kwa mti mkavu?! Ndivyo inavyoweza kutafsiriwa kwa Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference, TEC), Padri Anatoly Salawa kufuatia kunaswa kichakani akiwa na mrembo.

Kiongozi huyo wa dini alinaswa hivi karibuni majira ya saa 8: 02 usiku akiwa ndani ya gari aina ya Toyota RAV 4 lenye nambari ya usajili T 674 ADA kwenye kichaka kilichopo maeneo ya viwanda na gereji za magari makubwa, Kurasini jijini Dar.

Huku mvua kubwa ikinyesha na baridi ikipuliza vilivyo achilia mbali baadhi ya maeneo ya jiji kutotulia kwa mafuriko na foleni, waandishi wetu  walipigiwa simu na mlinzi mmoja wa Kimasai wa kwenye gereji hizo na kunyetisha juu ya gari lililosimama karibu na eneo lao la lindo huku likinesanesa.

Mlinzi huyo alieleza kuwa yeye na wenzake walilichunguza kwa makini gari hilo na kuona kuwa ndani yake kulikuwa na watu wawili wa jinsi tofauti lakini walishindwa kujua wazi kilichokuwa kikiendelea.

Mlinzi huyo alisema kuwa mara kwa mara gari kama hilo  limekuwa likifika hapo majira ya usiku wa manane hivyo kuwafanya kuingiwa na shaka.

Waandishi walifika eneo la tukio ndani ya muda mfupi na kuwakuta polisi nao wakiwasili kisha kuchukua kwanza maelezo kwa walinzi hao bila kuwashtua wahusika kwenye gari.

Baada ya mahojiano na walinzi hao, walilifuata gari hilo na kulipekua ambapo hawakuamini macho yao baada ya kumkuta mtu mzima huyo katika gari hilo akiwa na mrembo aliyekuwa mtupu.

Huku mvua ikiendelea kumwagika, padri huyo alionekana akiwa ametaharuki ndani ya gari asijue la kufanya.

Mara baada ya kuwanasa wawili hao, padri alijitetea kwa kusema kuwa, alikuwa ameingiliwa na wahuni katika starehe zake hivyo aliingia kwenye gari na kutimua na mrembo wake.

Jana  padri  huyo  alitafutwa  tena ili kama ana la ziada la kusema alitoe lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na baadaye ikazimwa kabisa.

Baada ya muda simu hiyo iliwashwa tena na ndipo  alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (SMS) . Hata hivyo, SMS hiyo haikujibiwa.


Baada ya SMS hiyo, padri huyo aliendelea kupigiwa simu lakini bado iliita bila kupokelewa ndipo akatumiwa ujumbe mwingine uliosomeka hivi; ‘mkuu tumepata tukio lako ukiwa kichakani ndani ya gari usiku na mrembo akiwa mtupu. Wewe unalizungumziaje tukio hili? Kwa maana nyingine unajiteteaje? Tunaomba maelezo yako’.

Kama ilivyokuwa kwa ujumbe wa kwanza, nao huo haukujibiwa.

Chanzo:  Gazeti  la  Ijumaa/Gpl

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu alivyotumba binadamu katukadiria kwa hiyo huduma ya mwili muhimu
    zingine kujitakia tu

    ReplyDelete

Top Post Ad