Shishi 'kubananishwa' na BASATA kwa kukiuka maadili..Akitua tu Nchini Anatakiwa Akajieleze

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia kusambaa kwa picha zinazoonyesha sehemu kubwa ya maungo ya mwili wa msanii wa muziki Shilole kutoka katika onesho lake alilofanya hivi karibuni huko Ubelgiji, msanii huyo anatarajiwa kulitolea ufafanuzi suala hilo mbele ya BASATA.

Shilole a.k.a Shishi Baby

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza, kitendo cha Shilole kufanya vitendo vya kudhalilisha hadharani, si mara yake ya kwanza kufanyika na Baraza hili lilikwishamwita kumuonya.

Taarifa hiyo inaweka wazi kuwa, msanii huyo atakaporejea nchini, litachukua hatua zifuatazo.
1. Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla
2. Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si sanaa na hakuna uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua.
Msanii huyo pia kwa upande wake anasubiriwa kwa hamu kutolea ufafanuzi wa kile kilichotokea kwa mashabiki wake Afrika Mashariki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad