Sikubaliani na Hoja ya LOWASSA Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dr.Slaa pengine ndiye mwanasiasa wa upinzani anaeheshimika na kusikilizwa zaidi Tanzania.

Yote hii ni sababu ya misimamo yake kupinga ufisadi, kusimamia na kutetea maslai ya Taifa bila kuogopa.

Amewahi kutaja hadharani listi ya mafisadi 11 Lowasa akiwa namba tisa na Kikwete akiwa namba kumi na moja.

Alienda kule Arumeru alimtuhumu Lowasa waziwazi kwa ufisadi na kukwepesha miradi ya Arumeru na kuipeleka Monduli.

Lakini leo tunaambiwa kuwa Lowasa anakaribishwa ndani ya Chadema na kuungama dhambi na atasamehewa.

Sina tatizo na ujio wa Lowassa ndani ya chama tatizo langu ni heshima na taswira ya Dr. Slaa aliyojijengea kwa muda mrefu kwa kuukemea ufisadi.

Je leo yupo tayari kutangaza hadharani kuwa Lowasa amekuwa msafi sio fisadi tena, yupo tayari kupunguza ile list of shame ya Mwembeyanga kutoka kumi na moja na kubaki kumi.?

Japo siasa hazina adui wa kudumu wala urafiki wa kudumu, kwa hili naona heshima ya Dr.Slaa na Chadema kwa ujumla ikiporomoka.

Maana heshima ya Dr Slaa na Chadema imejengwa kwa kuukemea ufisadi, lakini tunakoelea Hali itabadilika na kuwa Chadema ni chama cha kuwasafisha Mafisadi.

Nb.Ni mtazamo tu wadau msijenge chuki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Binafsi nilihuzunika sana mheshmiwa low as a kukosa kupeperusha bendela.. Nilikua mkereketwa wake haswaaa. But hill LA yy kutoka kaenda ukawa ilimradi tu aupate huo urais, nimetokwa na imani nae, ni wazi yupo kwa maslah binafsi na c ya wananchi.. Kwa upande wao nap ukawa wameonyesha udhaifu wa hali ya juu kabisa, hivi nowanachama wangapi wameipigania chadema kufika hapo ilipo? Kumbe cku zote hawakua na MTU mmaking wa kupeperusha bendela mpaka.. Yaani wao ndo walikua wananipa matumaini ila na nagundua ni bure kabisa... Kwa ubabaikaji juu CCM haitatoka madarakani mpaka cku jeshi litapoamua kufanya mapinduzi, wrote bure kabisa!

    ReplyDelete
  2. Lazima niwe rais tu ili malengo yangu yatimie , nitamnunua ukawa na watoto wake wote

    ReplyDelete
  3. Tobaaaaa yarabi

    ReplyDelete
  4. Jamani fedha fedheaaaaa,ukawa wamenunuliwa wote na sasa wamebaki kuwa ukiwa.
    Chezea pesa weweeeee

    ReplyDelete
  5. Umefika wakati kwa watanzania kufungua macho,wanasiasa wenye maslahi binafsi na vyama vinavyoshindwa kujisimamia tuviogope kama ukoma! hapendezi wala haifurahishi ukigeugeu unaoendelea.

    ReplyDelete
  6. Ehh......kumbe mtu unakuwa fisadi pale tu unapokuwa nje ya chadema,,,,,,,?nilikuwa sijui....ngoja nami niibeee,wakianza kunistukia naamia chadema.

    ReplyDelete
  7. Mpaka sasa nabadili mawazo,, bora nipigie kura yangu ACT kwa nguvu moja....... UKAWA hawakuwa na mgombea. Hata wakienda IKULU system itakuwa ile ile ya CCM... Wote ni mafisadi wasio na aibu

    ReplyDelete
  8. CCM OYEEEEEEEEEEEE!
    MAGUFULI YULEEEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  9. Ni shidaaaaaaaasas

    ReplyDelete
  10. Ni shidaaaaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad