Nape Asema Wanaohama CCM ni sawa na Mafuta Machafu.......Amtakia Kila la Heri Edward Lowassa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema wanachama waliokihama chama hicho wamejivua nguo mbele za watu na kwamba wapinzani wanaowachukua wanahangaika na mafuta machafu.

Aidha, amesema aliyekuwa Mbunge wa Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Milton Mahanga, alikuwa anatafuta sababu za kuihama CCM na anamtakia kila la heri, yeye na rafiki yake, Edward Lowassa.

Nape aliyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam, alipotakiwa kueleza kuhusu kuhama kwa Lowassa na Dk Mahanga ambao wote kwa nyakati tofauti wamekimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Lowassa alijitoa CCM wiki moja iliyopita baada ya kukwama uteuzi wa CCM wa kuwa mgombea wake wa urais na kukimbilia Chadema ambako anatarajiwa kuwa mgombea wake wa urais na kuungwa mkono na Umoja wa Vyama vinne vya Upinzani (Ukawa).

Dk Mahanga naye alijitoa juzi baada ya kukwama katika kura za maoni jimboni Segerea. “Wanahangaika na oil chafu. Hawa ni wale wale kama ilivyokuwa Mrema (Augustino) mwaka 1995, akabebwa kiasi cha Mwalimu Nyerere kusema mwacheni abebwa.

"Hebu jiulizeni wanaona ubaya wanapotoka, lakini mambo yakiwanyookea hawasemi, wakitoka ndio maneno mengi,” alisema Nape.
 
Alisema kuondoka kwa Lowassa na wengine wachache, si jambo la kwanza kutokea CCM, na pia si la ajabu wala haliwezi kuwa la mwisho huku akimtuhumu Dk Mahanga kuwa alikuwa akitafuta sababu ya kuondoka CCM.

Akizungumzia mchakato wake Mtama, Nape alisema kulifanyika juhudi kubwa za mafisadi kuhakikisha anashindwa, lakini anashukuru ameshinda na kwamba endapo atapitishwa na chama hicho kugombea ubunge, ana hakika atashinda kwani ni mwadilifu na anayezingatia ya chama hicho ikiwamo kupiga vita rushwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. INATOSHA NAPE!!Watanzania wengi wameichukia ccm kwa kuwa tu
    viongozi wao wengi hawana uchungu na walio chini,ambao ndio walipa kodi wanazozitafuna bila aibu.Watanzania wa chini wanakufa mahospitalini kwa kukosa pesa za matibabu,watoto wao wamefaulu lakini wanakosa vyuo kwa kukosa mikopo.Tanzania ina utajiri wa kutosha lakini hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku.Jamani tumehadaika vya kutosha na ccm na sasa ngoja tuone mabadiliko kwa chama kingine.

    ReplyDelete
  2. Ningemuona wa maana kama yasingekuwa yanatokea haya yanayotokea sasa ndani ya ccm!! kila kona ni wizi wa kura za maoni na njia inayotumika kufanya wizi huo!! kumbe ndio maana huwa wanatamba sana eti tutashinda kwa kishindo!! kumbe wanakuwa tayari na kura zao zilizo pigwa kabisa!!! nina wasi wasi watatumia njia hii hii kumuhujumu Lowasa!! nimewaogopa kama ukoma mwe!!

    ReplyDelete

Top Post Ad