UKAWA Kuzundua Kampeni Kesho Bila Dr. Slaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MRATIBU wa Maandalizi ya Kampeni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Deogratia Munishi amesema maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni yamekamilika kwa asilimia 90.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja hivyo vya Jangwani, Munishi amesema kila kitu kipo tayari katika maandalizi hayo na wanachosubiri ni mkutano.

Munishi amesema mkutano huo wa ufunguzi wa kampeni umepangwa kuanza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 12 jioni.

Amesema, mkutano utahudhuliwa na watu kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwemo wanachama kutoka nje ya nchi kama Zambia na sehemu nyingine duniani.

Aidha, amewataja viongozi watakaohutubia katika mkutano huo kuwa, Mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, Mgombea Mweza, Juma Duni Haji, viongozi wakuu wa UKAWA na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali.

Kuhusu uwepo wa wasanii katika mkutano huo amesema: “Wasanii watakuwepo lakini hawatapamba mkutano kama kule kwa wenzetu, sisi tunakuja kutangaza sera na sio tamasha la wasanii.”

Naye Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ametoa ratiba ya Mgombea urais na mgombea mwenza kuwa, mara baada ya uzinduzi wa kampeni hizo wataanza ziara mikoani.


Amesema Lowassa, Jumapili ataanza ziara yake Mkoani Iringa na kufanya mikutano ya hadhara minne ambapo ataanzia Mufindi, Kilolo, Karenga, na Iringa Mjini kila sehemu mkutano mmoja.

Kwa Upande wa Babu Duni, amesema ataanzia Mtwara katika wilaya ya Newala, Tandahimba, Mtwara vijijini na Mtwara mjini.

Aidha, kuhusu tetesi za uwepo wa Katibu mkuu Chadema, Dk. Willbrod Slaa viwanja vya jangwani Makene amesema: “Hizo ni tetesi tu. Hakuna ukweli wowote. Dk. Slaa (Willbrod) amepumzika acheni kumzushia maneno.”

Ameongeza, mkutano utakuwa laivu katika televisheni na radio zisizopungua tano kuanzia saa 9 hadi 12 jioni.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Muziki mzito huo,ukoo wa panya a.k.a c..m lazima waumie mwaka huu.

    ReplyDelete
  2. Ukiweka fact kila mtu anasepa nocomment tunapiga kimya,,,,,lakini kwani DR Slaa peke yake ndiye anaye uliziwa kwani Profesa Lipumba je? Yeye atakuwepo?

    ReplyDelete
  3. Kwani Slaa yeye nani

    ReplyDelete
  4. Tunasonga mbele

    ReplyDelete

Top Post Ad