Lilian Kamazima: Najuta Kubeba Taji 2015

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mrembo wa Tanzania 2014-2015, Lilian Kamazima amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa kuna kipindi anajuta kwa nini alijiingiza kwenye mambo ya urembo kwa mwaka huo kwani hakufaidi nafasi hiyo kutokana na adhabu ya kufungiwa ambayo ilimuathiri sana.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Lilian alisema kuwa mara nyingi unaposhiriki unakuwa na matumaini ya kushinda na baada ya hapo uweze kufanya vitu vingi kwa jamii yako kama inavyotakiwa kwani hata waliopita walifanya hivyo, lakini inapokuja kinyume huwezi kuwa sawa.

“Nilipopata taji la urembo kutoka kwa Sitti, nilikuwa na malengo mengi sana kwa jamii yangu kama walivyofanya warembo wengine, lakini nilishindwa kwa sababu ya kufungiwa kwa mashindano hayo kwani hata kama ningeamua kufanya jambo fulani nisingeweza kwa kuwa ningetamka natokea Miss Tanzania nisingepewa msaada,” alisema Lilian.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad