Picha za Kwanza Kutoka Kwenye Tukio la Ajali Lililochukua Maisha ya Mchungaji Christopher Mtikila

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP), Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani alfajiri ya leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 alfajiri ya leo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari alilokuwa amepanda Mtikila lilikuwa linatoka mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya na kupelekwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha, Pwani kwa matibabu.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia habari zetu tutakujuza hivi punde.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mapenzi ya MUNGU ndio maana tunaambiwa tukeshe kwani hatujui siku wala saa pole kwa familia

    ReplyDelete

Top Post Ad