Uwezo wa Rais Magufuli Kupambana na Dawa za Kulevya Wahojiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Madawa ya Kulevya
RAIS mpya wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameambiwa kama ni kweli amenuia kukomesha biashara ya madawa ya kulevya nchini, basi awashughulikie wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza bidhaa hiyo.

Anaweza kuanza kwa kuifanyia kazi orodha ya wafanyabiashara 104 magwiji wa madawa hayo, orodha ambayo alipewa mtangulizi wake, rais mstaafu Jakaya Kikwete alipoingia madarakani Desemba 2005.



Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya madhehebu ya dini nchini, Askofu William Mwamalanga amesema orodha hiyo iliguswaguswa tu na uongozi uliopita.

?Sisi viongozi maaskofu na masheikh 120 tuliokutana kwa siku tatu mjini Arusha kwa lengo la kutathmini athari za tatizo la matumizi ya mihadarati kwenye Nchi za Maziwa Makuu, tunampongeza Rais John Magufuli kwa kuweka wazi ajenda ya kupambana na janga hili nchini. Tunamhimiza aishughulikie ile orodha tuliyomkabidhi mtangulizi wake,? amesema Askofu Mwamalanga.

Hayo yamo katika tamko la kongamano lililoshirikisha viongozi wa dini wa nchi za kanda ya Maziwa Makuu kwa ushirikiano wa mashirika ya kidini ya Ujerumani, Marekani na Afrika yanayopambana na biashara ya usafirishaji, usambazaji, utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana katika nchi za Ulaya na kanda hii ya Kusini mwa Afrika.

Tunaungana naye katika kusimamia ajenda aliyoitangaza katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 11; tunadhani wakati umefika awezeshwe kutungwa sheria ya adhabu ya kifo ya kuwashughulikia wafanyabiashara wakubwa wa unga kama ilivyo nchini China. Atakuwa ametoa mchango muhimu katika kupunguza uharibifu unaofanywa dhidi ya maelfu kwa maelfu ya vijana wa Afrika, wakiwemo Watanzania.

Askofu Mwamalanga wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste ameonya Tanzania ni muathirika mkubwa wa tatizo hilo kwa miaka mingi sasa kama ilivyo kwa janga la rushwa na ufisadi, na kusisitiza panahitajika sheria hiyo ishikiliwe kwa uimara.Amesema hotuba za maneno matupu haziwezi kutokomeza rushwa na biashara ya mihadarati kwani wamiliki wakubwa ni watu wenye utajiri mkubwa kwa hivyo moyo alioonesha rais mpya utakuwa ukombozi.

Mwanzoni mwa mwaka 2006, Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya madhehebu ya dini nchini ilikutana na Kikwete na kumkabidhi orodha ya magwiji 104 wa mihadarati ?kiukweli hapajawa na mafanikio kwani leo miji yote Tanzania vijana wanafanyabiashara hiyo kama njugu.?

Askofu Stave Marks na Profesa George Furhaman kutoka Ujerumani wametambua mchango wa Kamati ya Askofu Mwamalanga wa kukabidhi orodha ya magwiji wa mihadarati kwani Tanzania haipaswi kutumiwa kama uchochoro wa kupitisha bidhaa hiyo kwa asilimia 11 kwenda nchi za Kusini mwa Afrika na Ulaya.

Orodha hiyo inajumuisha majina ya watu waliokuwa wakitumia mgongo wa vyeo na nafasi zao serikalini na pia ukaribu wao na viongozi wakuu na marais wa mataifa mbalimbali ya Afrika Tanzania wakiwemo maaskofu, wachungaji, manabii na masheikh wa uongo.
Mbele ya kongamano hilo, Padre kutoka Zambia alikiri kuwahi kuwa kinara wa mtandao mahsusi wa kusafirisha madawa ya kulevya kupitia Dar es Salaam, Tunduma, Lusaka na kuingia Afrika Kusini kati ya mwaka 2005 na 2007.

Alidai kuiacha kazi hiyo baada ya kubaini kuwa jina lake lilikuwemo kwenye orodha aliyokabidhiwa Kikwete mwaka 2006 na amesema walioamua kuacha kama yeye ni mashujaa kwani wengi wao wameishia kunyongwa nchini China.?
Masheikh Abdallah Zuberi wa Mombasa na Kassimu Mohmed wa kisiwani Pemba ameitaja Zanzibar kama kitovu kikubwa cha mihadarati kwenye ukanda huu kutokana na usimamizi dhaifu wa sheria.

Sheikh Mohamed amesema kama jitihada za kudhibiti viongozi wakubwa wanaoendeleza biashara hiyo zitaachwa kwenye ahadi za wanasiasa walioko madarakani, ipo hatari kwa nchi nyingi za Afrika kuongozwa na magwiji wa unga hasa kwa kuwa safari hii wapo baadhi yao wameshinda uchaguzi mkuu na kuingia bungeni.

Amewataja watu wanane alioita mapapa wa biashara hiyo wanaoishi Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar, aliosema wamewatia mfukoni viongozi wakubwa waliochaguliwa ndipo serikali ikabaki kuhimiza tu katika danganya toto huku ikiichezea orodha.

Chanzo: Mitandaoni


Je Unatafuta Ajira Ama Unataka Kubadili Kazi Uliyonayo?
Basi Bonyeza: Ajirayako.com


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Majina aliyokuwanayo kikwete yako wapi

    ReplyDelete
  2. ATAKAPO KAMATWA BABA'KO NDIO UTAJUA KAMA NI DAGANYA TOTO AU DANGANYA KUBWA

    ReplyDelete

Top Post Ad