Askari wa Kike wa Usalama Barabarani na Mpenzi wake Waungua moto Hadi Kufa Kisa Hichi Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Picha ni ya Tukio jingine la Moto
Askari wa kike wa Usalama Barabarani, Attuganile Mwakibete (37) na mpenzi wake Sunday Mhagama (36), wameteketea kwa moto baada ya nyumba walimokuwa ndani kuungua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema tukio hilo lilitokea Februari 2, mwaka huu saa 7:15 mchana katika kitongoji cha Maporomoko, Kata na Tarafa ya Laela Wilaya ya Kipolisi ya Laela.

Inadaiwa kuwa nyumba hiyo iliyoteketea kwa moto ambayo askari Attuganile alikuwa amepanga vyumba viwili, ni mali Yaiyela Mwamahonje aliyokuwa akiishi na watoto wake wawili wadogo ambao wamenusurika kufa, licha ya kuwemo ndani ya nyumba hiyo wakati wa ajali hiyo.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Mhagama aliyekuwa rafiki wa trafiki huyo wa kike, ni mkazi wa Mbeya ambako mkewe anaishi, na alikuwa na mazoea ya kumtembelea mpenzi wake huyo mara kwa mara.

Inadaiwa askari Attuganile alikuwa ameachana na mumewe wa ndoa. “Vyumba viwili yaani sebule na chumba walimokuwemo Attuganile na Mhagama viliwaka moto baada ya jenereta lililokuwa likifanya kazi likiwa sebuleni humo kulipuka na kuwajeruhi vibaya,” alieleza.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, Attuganile alifariki dunia Februari 8, mwaka huu saa 2:30 asubuhi akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga.

Mhagama alikimbizwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya jijini Mbeya ambako alifariki dunia Februari 9, mwaka huu. Kamanda Mwaruanda alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mshahara wa dhambi ni mauti!!!

    ReplyDelete
  2. Mshahara wa dhambi Ni mauti

    ReplyDelete
  3. Uongo hiz pic ni za nyumba iliyoungua bugurun ikateketeza familia nzima

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inawezekana picha hizo zimetumika kama mfano tu na tukio hilo limetokea kweli huko Sumbawanga.

      Delete

Top Post Ad