Mamluki Waliobaki Ndani ya CCM Siku zao Zinahesabika..Jakaya Kikwete Aagiza Waanze Kushughulikiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MAMLUKI waliobaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), siku zao zinahesabika, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, kumuagiza Makamu Mwenyekiti, Tanzania Bara, Philip Mangula kuanza kuwashughulikia.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya 39 ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Namfua, mkoani Singida, Kikwete alisema chama hicho kimevuka salama katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba mwaka jana, pamoja na baadhi ya wenzao kuondoka.

“Tunashukuru uchaguzi ulipita na Chama kimevuka salama katika mchakato mzito kinyume na watu walivyotutabiria kifo… haukuwa rahisi kwetu kwa sababu ulizidiwa na kelele na vitisho pamoja na kuwepo wenzetu waliotuhama na kudhani tutakufa lakini hatukutetereka.

“Tunajua wako wengine waliobaki kama mamluki, lakini wajue siku zao zinahesabika maana hatutakubali kuendelea kunyonywa damu, natumaini Mangula umeanza kuwashughulikia hawa mamluki,” alisema Mwenyekiti huyo anayemaliza muda wake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. haya sasa mzee wa mipasho, rais mtalii mstaafu uliyemwachia jembe wetu jpombe kazi kubwa ya kurudisha mamilioni uliyoyateketeza wewe ndiye mamluki namba one na siku zako zimeisha kaa pembeni acha tingatinga awe huru.

    ReplyDelete
  2. Hahaaa yepp... the kenge has spoken. Umpe ruhusa na halfani amtembelee baba yake nguza angalau mara moja kwa mwezi....

    ReplyDelete
  3. mzushi kaa pembeni tuachie pombe wetu asafishe uozo ulioacha

    ReplyDelete
  4. mzushi kaa pembeni tuachie pombe wetu asafishe uozo ulioacha

    ReplyDelete
  5. Ndo maana Singida tulikataa kukupa mke hufai

    ReplyDelete

Top Post Ad