Chozi la Mobeto Laana Kwa Lulu Michael

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kudaiwa kumpora mwanaume aliyezaa naye, chozi la mwanamitindo anayeuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Hamisa Hassan Mobeto linaelezwa kuwa ni laana tosha kwa mwigizaji huyo.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Mobeto, mrembo huyo ambaye ni sura ya mauzo kwenye matangazo ya nguo za kike, amekuwa akimwaga chozi kila kukicha huku lawama zote akizielekeza kwa Lulu.

Chanzo hicho kilidai kuwa, Mobeto amekuwa akilalamika kwamba, Lulu alijua fika mwanaume huyo ni mzazi mwenzake lakini akamchukulia na kumsababishia maumivu ya kutelekezewa mtoto wa kike aliyezaa na jamaa huyo mwaka jana.

“Kiukweli chozi la Hamisa (Mobeto) kila kukicha ni laana tosha kwa Lulu. Unajua hakuna kitu kibaya kwa mwanamke kama kuporwa mwanaume wake waziwazi na kuachiwa majukumu ya mtoto huku adui ukimjua.
“Kibaya zaidi ni tambo za Lulu mitandaoni. Kitendo cha Lulu kutamba na mwanaume huyo kinamuumiza sana Mobeto kwa sababu naye ni mwanadamu. Ana moyo wa nyama kama Lulu

“Pia ukiacha tambo, Lulu amekuwa akisababisha mtoto wa Mobeto anatukanwa jambo lililomuongezea machungu kwani mtoto ni malaika ambaye hajui chochote lakini amekuwa akiunganishwa kwenye ugomvi huo,” kilieleza chanzo hicho.
Alipotafutwa Mobeto hivi karibuni kuhusiana na sakata hilo, hakuwa tayari kumzungumzia Lulu na mwanaume huyo lakini akaweka wazi kwamba kinachomuumiza ni mwanaye kuhusishwa na ugomvi huo.

“Ishu ya Lulu na …(anamtaja mwanaume) siwezi kuizungumzia, kitu ambacho kinaniumiza ni kumwingiza mwanangu kwenye haya mambo. Mtoto wangu anakuwa anajumlishwa katika mambo ambayo hayamuhusu kabisa na hakupaswa kuhusishwa,” alinukuliwa Mobeto na kuongeza:
“Hakuna mzazi ambaye angekubali mwanaye aongelewe kwenye mambo yasiyo mazuri. Ningekuwa sina mtoto wala nisingeumia lakini kwa sababu kuna mtoto ambaye hana hatia wala hajui kinachoendelea hivyo sipendi na naumia sana.”
Jitihada za kumpata Lulu ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS na chatting za WhatsApp hakujibu.

Ishu hiyo ya laana kwa Lulu ilipigiliwa msumari na mama wa marehemu Steven Kanumba alipozungumza na wanahabari wetu hivi karibuni katika futari iliyoandaliwa na mwigizaji Illuminata Poshi ‘Dotnata’, nyumbani kwake, Ubungo jijini Dar.
Alisema Lulu analiliwa na wanawake wengi kwani wapo ambao alikuwa na uhusiano na waume zao wakafariki dunia huku wengine wakiachwa na watoto wadogo na kubaki wakilea wenyewe.

“Lulu ana machozi ya wanawake wengi, Mungu anaona na ninaamini machozi hayo hayataenda bure ipo siku atakuja kuvuna anachopanda kwa sasa,” alisema mama Kanumba pasipo kutaja wahusika moja kwa moja.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na kweli Lulu utakuja kuvuna unachokipanda kumchukulia mtu bwana ambaye amezaa nae ni kosa kubwa sana kuna leo na kesho ipo siku jamaa atakuchoka atachukuwa demu mwingine mrembo zaidi yako na wewe utakuja kumwaga machozi kila siku na muda si mrefu kwani nawajua wanaume wakibongo wanatamaa hawawezi kuwa na demu mmoja kwa muda mrefu, tena yatakayokutokea wewe ni mabaya zaidi na yaliyomtokea Hamisa sababu una laana za watu wengi, wewe cheka leo kesho na keshokutwa utakuwa wewe ni mtu wa kulia tu na ngoja uataona na utakumbuka nilichoandika

    ReplyDelete
  2. Kuzaa si tija
    Kwani kaolewa ?
    Mwanamke shughuli bibi
    Kwani mlikuwa hamjui
    Mwanaume udugu wa nazi kwenye pakacha
    Kama hukuchuna afajiri kwa buzi magharibi utambulia supu ya kwato za mbuzi
    Ulizeni manyakanga wawafundeni
    Hamuachi

    ReplyDelete
  3. kweli kabisa jamani lulu acha izo tabia, we mbona mdogo saana lakini umebeba m zigo mkubwa wa wanaume za watu kumbuka ipo siku ukiwa na mji wako hutakuwa salama kabisa utajuta haya yote yatakurudia. kwani huwezi kuiba mume wa mtu kwa siri lakin wewe unataka hadi kuku wafahamu kama unadet na fulani? mungu atakuacha salama yatakupata kama ya amini chifupa maana unavuma kama chumvi sio vizuri mtoto mdogo kama wewe

    ReplyDelete
  4. badili ya mwanaume ni mwanaume you are still young and beatiful why are you bothering songa mbele first of all lulu she is not beatiful at all bahati tu lakini penye wazuri yeye sio mzuri without make she is nothing kama kawaida but look at yourself Hamisa you are mwa mwa

    ReplyDelete
  5. Kesi yake vipi ?

    ReplyDelete

Top Post Ad