Viongozi Mbalimbali wa Chadema Waendelea Kutiwa Mbaroni Kwa Uchochezi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zikiwa zimesalia siku nne kabla ya maandamano yanayodaiwa yatafanywa na Chadema, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekuwa kiongozi wa 26 wa chama hicho kukamatwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi ndani ya kipindi kifupi.

Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na kauli zao zinazosisitiza kufanyika kwa maandamano yaliyopewa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), yaliyopangwa kufanyika nchi nzima Septemba Mosi.

Hata hivyo, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imezuia maandamano hayo na mikusanyiko yoyote ya kisiasa hadi mwaka 2020 kwa lengo la kuipa nafasi Serikali iliyopo madarakani kuwaletea wananchi maendeleo.

Baadhi ya viongozi wa Chadema waliokamatwa na kuhojiwa mpaka sasa ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Visiwani, Salum Mwalimu, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye kesi yake iko mahakamani.

Lissu alikamatwa Agosti 3, mkoani Singida baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi uliopo jimboni kwake kwa tuhuma za uchochezi.

Agosti Mosi, Mbowe alijisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na kuhojiwa kwa saa tatu. Kiongozi huyo aliitwa kwa mahojiano maalumu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kauli za chama hicho kukinzana na agizo la Rais John Magufuli la kuzuia shughuli zozote za kisiasa ikiwapo mikutano kufanyika nchini.

Lema alikamatwa juzi alfajiri nyumbani kwake Njiro kwa Msola na makachero wa polisi kwa tuhuma za uchochezi ikiwa ni siku moja tangu kuachiwa kwa dhamana Diwani wa Chadema wa Kata ya Sombetini, Ally Benanga aliyefunguliwa mashtaka ya uchochezi mahakamani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo jana alithibitisha kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea wa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi mitandaoni.

Alisema mbunge huyo alitoa kauli za uchochezi na kuzisambaza kwenye mitandao, mapema wiki hii.

Polisi walisema ujumbe wa Lema kwenye mtandao ulisisitiza wito wa kufanyika mikutano na maandamano ya Ukuta, kwamba Mkoa wa Arusha umejiandaa kwa lolote na yeye atakuwa mstari wa mbele.

Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro alithibitisha kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa bado walikuwa hawajajua tuhuma zake.

“Ni kweli mbunge anashikiliwa na tunaendelea kuhangaika apate dhamana leo (jana), ama afikishwe mahakamani,” alisema.

Salum Mwalimu na wenzake 17 watiwa mbaroni
Wakati Lema anakamatwa Arusha, Naibu Katibu Mkuu Visiwani, Salum Mwalimu na wenzake 17 walikamatwa wakati wakijiandaa kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 25, saa 10 jioni katika kijiji hicho.

Lyanga alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wanajiandaa kufanya mikutano ya hadhara yenye lengo la uchochezi.

Alisema baada ya kupata taarifa kutoka katika vyanzo vyao, walifika eneo la tukio na kuwakamata kwa kuwa hata kibali cha kufanya mkutano hawakuwa nacho.

Jana, Mwalimu na wenzake walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi na kusomewa mashtaka ya kuwashawishi wananchi kufanya vitendo viovu na uchochezi.

 Viongozi hao walinyimwa dhamana na kurudishwa rumande hadi Agosti 30.

Agosti 23, Diwani wa Chadema, Kata ya Sombetini, Ally Bananga (40), alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kujibu tuhuma za kuhamasisha uchochezi.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi Augustino Rwezire, diwani huyo alidaiwa kuhamasisha wananchi kufanya maandamano yasiyo halali, Septemba Mosi.

Diwani huyo alifikishwa mahakamani hapo Agosti 23, ambapo Wakili wa Serikali Charles Kagirwa, alidai alitenda kosa hilo Agosti 13, wilayani Karatu Mkoa wa Arusha.

Pia, alisema kuwa siku ya tukio Bananga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa wazi uliofanyika eneo la Hosteli ya Karatu, aliwahamasisha wananchi hao washiriki katika kusanyiko lisilo halali Septemba Mosi.

Agosti 25, viongozi wengine wanne wa Chadema Jimbo la Kigoma Mjini, walikamatwa na polisi wakidaiwa kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

Waliokamatwa ni mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Kigoma, Ally Kisala, Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Mkoa (Bavicha), Omary Gindi, Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na Mwenyekiti wa mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (DCP), Ferdinand Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda lakini walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti kituoni hapo jana.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kigoma, Shaaban Madede aliwaomba Polisi kwamba chama hicho kimejipanga kuandamana kwa amani na kufanya mikutano kila pembe ya mkoa, lengo ikiwa ni kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya kilio chao dhidi ya Serikali kukandamiza demokrasia.

Wabunge CUF  Waunga Mkono UKUTA
Wakati wabunge wa Chadema wakikamatwa, wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), wamesema wanaunga mkono Ukuta, kwa sababu imelenga kupambana na uvunjaji wa demokrasia unaodaiwa kufanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Msimamo huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Wabunge wa CUF, Riziki Mngwali alipozungumza na wanahabari kufuatia taarifa zilizosambaa kuwa wabunge hao wanapinga Ukuta.

Riziki ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, alisema wabunge wa chama hicho hawana tatizo na Ukuta na wanaunga mkono, hivyo tofauti na propaganda zinazoenezwa kuwa wanaupinga.

“Chadema ni washirika wetu kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hivyo hatuna sababu ya kutowaunga mkono.

 “Tunachosubiria ni taratibu za uongozi wa juu kukamilika kisha watupe mwongozo nini cha kufanya kwenye Ukuta. Lakini wabunge tupo pamoja na operesheni hii, hatuipingi kwa sababu ina lengo ya kudai haki na demokrasia inayominywa,” alisema Riziki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watakamata wengi
    Lakini ukuta Upo pale pale
    Kama wana ubavu wanikamate miye
    Tarehe 01.09
    Watanzania dunia nzima
    Tuandamane
    Kwa walio nje ombeni vibali mwende ofisi za balozi zote Tanzania
    Tuwaambie dunia hali halisi ya awamu ya Tano
    Kwa walio nje it's simple
    Iteni CNN na BBC and local tv

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe mnafiki uliyoandika yanakufaa mwenyewe eti ukamatwe wewe tarehe 1. 09 ili wasioukuwa na akili kama wewe watoke wakaandamane wakati tarehe hiyo wewe utakuwa umeshinda chini ya uvungu wa kitanda umejificha

      Delete
  2. Mtakamata wengi
    Lakini ujumbe umefika
    Mtajifanya mabubu
    Mnajuwa
    Hamkisolewi
    Hamshauriki
    Lakini nguvu umma ipo siku itakuwa
    Na nyinyi
    Polisi
    Wanajeshi
    Kushabikia CCM
    Yote yanamwisho
    Watanzania muuishio ughaibuni 01..09
    Andamaneni kuonyesha ulimwengu
    Tanzania Hakuna demokrasia
    Maanake hapa Tanzania jeshi la wanainchi lisha tangaza litafanya usafi kusherekea miaka 52
    Tanzania ya CCM kwa usanii
    Lakini hata wafanyeje
    Usilazimishe watu wakupende
    Watanzania wengi hatuna Imani tena na awamu hii

    ReplyDelete
  3. CHAMA CHA MAZINGAOMBWE27 August 2016 at 15:32

    TATIZO SIO UKUTA ,TATIZO NI MHE. RAIS MAGUFULI NA HOJA ZA KULETA MAENDELEO KWA KUZUIA WAJIBU NA HAKI ZA KIKATIBA?!!? SIJAWAHI KUSIKIA!!! NI MAENDELEO GANI TULIYOPATA KIPINDI CHA UWEPO WA CHAMA KIMOJA!!??. KAMA UMESHINDWA KULETA MAENDELEO NDANI YA MIAKA 50 ,UTAWEZAJE KULETA HAYO MAENDELEO NDANI YA MIAKA MITANO TENA KWA KUIONGOZA NCHI KWA PRESHA,HOFU,KUTOFUATA KATIBA WALA SHERIA NA KUTOA MATARAJIO HEWA!!.

    MPAKA SASA HAKUNA HATA UAMUZI MMOJA WA RAIS ULIOWEZESHA KUPATIKANA KWA UNAFUU WA MAISHA YA MTANZANIA WA KIPATO CHA CHINI. HAKUNA! KUANZIA KILIMO,UFISADI,BIASHARA,HAKI,MAENDELEO,DEMOKRASIA, N.K. HAKUNA!.

    KILA SIKU KILA SAA NI HABARI ZA POLISI NA MAAMUZI YA BWANA MKUBWA KWA KIGEZO CHA AMANI.AMANI TUNAYO NA HAITOTOWEKA NA HAKUNA MWENYE DHAMIRA YA KUVUNJA AMANI SIO CHADEMA WALA CCM.

    KINACHOFANYIKA NI CCM KUPITIA MSIMAMO BINAFSI WA RAIS KUTUMIA MWANYA WA MANENO KAMA; "UCHOCHEZI","MAENDELEO",N.K KWA MAMBO MAWILI: A) KUJIIMARISHA ZAIDI KISIASA NA KIUCHUMI HUKU VYAMA VINGINE VIKIFUNGIWA KUPATA HAKI HIYO KULINGANA NA KATIBA. B)KUENDELEA KUWEKA GIZA KWA WATANZANIA WENGI KATIKA KUWA NA UWEZO WA KUJIAMINI,KUJIELEWA,KUTAMBUA NA KUTETEA HAKI NA WAJIBU WAO KIKATIBA.


    ReplyDelete
  4. Maandamano ni kitu cha kawaida na uchochezi ni huu unaofanywa na CCM kutia ndani viongozi wa upinzani na Tanzania inapelekwa pabaya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe Harthy uchwara na shogako Salim Mwalimu kaane chini mujifikirie kiburi si maungwana mtoke kwenu huko kumetulia mtuletee balaa huku usukumani kama mnayataka hayo maandamano kaanzie kuhamasisha kwenu na nduguzenu na wake zenu mjitokeze kuandamana sio kuja kutulaghai kwa kutuona wajinga kisa ni wasukuma tuhimili hilo varangati la polisi kwenu wamewashinda

      Delete
    2. Wee Anonymous hapo juu inaonyesha wazi huna kisomo kutokana na kiswahili chako cha mitaani. Inabidi usome , ujikwamue kwanza ndipo ufunguke. Ni nyinyi Mizigo isiyo na elimu wala kujua sheria zenu za nchi. Hata ukiambiwa kunya utakunya.Elimu ni msingi wa maendeleo. Kosa kila kitu jielimishe ili utumie elimu yako kuandika mambo. Huwezi kumfundisha mjinga mpaka apate elimu. Na mmejaa wengi mno.

      Delete

Top Post Ad