TAARIFA Kuhusu Usalama Wa Dawa Aina Ya “Diclofenac” Na “Diclopar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


TAARIFA KWA UMMA    28  Oktoba, 2016
USALAMA WA DAWA AINA YA “DICLOFENAC” NA “DICLOPAR”

1. TFDA inajukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa dawa aina ya “Diclofenac” kupitia mitandao ya kijamii kama ilivyojitokeza mwaka  2013.

3. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda tena kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

a. Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs” (NSAIDs) ambazo hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na magonjwa mbalimbali kama magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi namaumivu ya kichwa.

b. Mamlaka imesajili dawa yaDiclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake na hivyo dawa ya Diclofenacinayotumika nchini ni salama kwa matumizi ya binadamu. Aidha, tunapenda kusisitiza kuwa dawa yenye jina la kibiashara la Dicloparina mchanganyiko wa viambato hai vya Diclofenac na Paracetamolimesajiliwa na TFDA na ni salama kwa matumizi ya binadamu.

c. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika ikiwa ni pamoja na kusababisha vidonda vya tumbo, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.

d. Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya(European Medicines Agency yenye makao yake jijini London, Uingereza)ilitoa tahadhari kwamba watu wenye matatizo  ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.

4. Kufuatia taarifa hiyo, sanjari  na mifumo ya ufuatiliaji wa madhara yatokanayo na dawa nchini, TFDA inaendelea kufuatilia madhara yatokanayo na dawa hii kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kitaalam ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Aidha, tunawakumbusha watoa huduma za afya kutoa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika vituo vyote vya afya nchinipamoja na kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki unaopatikana katika simu za mkononi aina ya “Android” kupitia anuani ya mtandao: www. tfda.go.tz/adr

5. Mamlaka inashauri watoa huduma za afya nchini na wagonjwa kuchukua tahadharizamadhara haya hasa kwa watu wenye magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari, wenye lehemu nyingi kwenye damu na wanaovuta sigara ikiwa ni pamoja na kutumia dawa mbadala.

6. Vile vile wananchi wanashauriwa kuepuka matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri wa kitaalam ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad