11 Jan 2017

Label Kubwa za Nje Zinazowasaini Wasanii wa Afrika Kwa Lengo la Kuwapoteza Kwenye Ramani ya Muziki⏩Rapper na mwanazuoni Nikki wa Pili, amefunguka kwa kudai kuwa label kubwa kutoka ugaibuni zinakuja Afrika kusaini wasanii kwa lengo la kuwanyonya na baadae kuwapoteza kwenye ramani ya muziki.

Rapper huyo wa Kundi la Weusi amezifananisha label hizo na makampuni ya madini kutoka Ulaya ambayo amedai mara nyingi yakuja nchi za Afrika kwaajili ya kupora rasilimali.
.
. “Ujio wa makampuni makubwa ya muziki Africa toka ugaibuni, hauna tofauti na makampuni ya madini, lengo ni lile lile uporaji..time will tell,” alitweet Nikki wa Pili.

Aliongeza kupitia Instagram kwa kusema, “Afrika Kusini na Nigeria muziki wao wameukuza na kuutangaza wenyewe, toka enzi za P Square mpaka Wizkid, au toka Marium Makeba mpaka Mafikizolo. Ujio wa wageni ndiyo unakuja kuushusha. Mtazame #Davido toka amesainiwa na Sony na kabla ya hapo au #Keko wa Uganda, au #RoseMhando. Hawa walisainiwa Sony na pili makampuni hayo lengo ni kufungua milango ya huku kwa muziki wa nje ndiyo maana Mtv Awards main artist alikuwa Future”


Hapa nchini Tanzania kwa sasa ni @officialalikiba pekee ndiyo ambaye yupo chini kampuni ya Sony.

⏩KARIBU KUTOA MAONI YAKO7


Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger