Gossip, Politics And Love Affairs

AMWAGIWA Tindikali Kisa Mapenzi...!!!


MATUKIO yanayohusiana na mapenzi yameendelea kuwa tishio nchini baada ya mwanamke mmoja, Helen John (25) kumwagiwa tindikali na mpenzi wake na kumfanya jicho lake lisione.

Hellen ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kwamhosi kata ya Nkumba wilayani Muheza mkoani Tanga, alipata mkasa huo Aprili 17, mwaka huu.

Akizungumza na Nipashe , alisema chanzo cha tukio hilo ni baada ya kukosana na mpenzi wake huyo na kufanya kuishi tofauti bila mawasiliano hadi siku ya tukio ingawa walikuwa wamezaa mtoto mmoja.

Hellen alisema siku ya tukio kijana huyo aliyemtaja kwa jina la Ally Khamis alikwenda nyumbani kwao kwa lengo la kumbembeleza kurudiana lakini alikataa kwa madai kuwa hataki kuishi na mwanaume huyo kutokana na vitendo vya ukatili ambavyo amekuwa akimfanyia.

Alisema baada ya kukataliwa kijana huo usiku alikwenda kumuwmwagia tindikali machoni na kisha kukimbia lakini ulifanyika msako kwa wanakijiji na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kupelekwa katika kituo cha polisi Muheza.

Credit - Nipashe
Tupe Maoni Yako
Lebel:

Post a Comment

[blogger]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget