Maadui Johari, Nora Wapatana, Wapanga Kurudi Kwa kasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mastaa wakongwe nchini, Nuru Nassoro, maarufu kama Norah, pamoja na staa mwenzie blandina chagula (Johari) sasa hivi mambo yamekua shwari baada ya bifu la muda mrefu kati yao. 

Chanzo cha bifu Lao ilikua ni mapenzi pamoja na shutuma za kurogana ,ambapo awali johari alikua akijiweka kwa muigizaji ray kigosi, then baadae ilikuja kubainika nora nae anajisevia kwa handsome boy huyo ambaye ni baba mtoto kwa sasa. 

Johari alivyokuja kugundua ikawa patashika nguo kuchanika, wakawa wananuniana na kutoleana vijembe, hali ikawa mbaya zaidi ambapo walimkosesha nora dili za kucheza filamu kwenye kampuni yao ya RJ, kitu kilichofanya nora apotee kabisa kwenye ulimwengu wa filamu. 

Norah alipoulizwa kuhusu ugomvi wake na johari, alidai tu ni wivu wa kijinga na aligundua staa mwenzie huyo na ray wanamroga kufifisha nyota yake pamoja na kumuaribia madili ya filamu kwa baadhi ya ma producer nchini. 

Hata hivyo sasa hivi wawili hao wanaonekana kupatana sana na kushirikiana kwenye baadhi ya mambo ya kijamii, pia tunategemea kuwaona pamoja wakiigiza kama ilivyokua awali, wote tunatambua umahiri wa johari na nora mbele ya camera,waswahili wanasema ,Old is Gold.

Baadhi ya movie za johari na nora zilizowahi kutikisa zamani ni JOHARI, DANGEROUS DESIRE,SIKITIKO LANGU na nyingine kibao.

Bado tunaamini vipaji vya dada zetu hawa,hivyo tunawakaribisha kwenye uwanja wa filamu kwa mikono miwili
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad