WALIOPINGA Wanyama Asipewe Mtaa Walisema si Uzalendo, Je Gor Mahia Nao si Wazalendo Kwa Kuita Tawa Lao Magufuli Huko Kenya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Timu ya soka ya Gor Mahia ya nchini Kenya ina matawi zaidi ya 400.
Katika matawi yote hayo hakuna hata moja lililopewa jina la Rais Uhuru Kenyatta, ila juzi wamezindua tawi jipya na kuliita tawi la Magufuli.

Waliopinga Wanyama asipewe mtaa walisema si uzalendo, Je Gor Mahia nao si wazalendo kwa kumpa Magufuli tawi?

Wajinga walishabikia Bango la Wanyama kung'olewa, Je KFF nao watangaze kulifuta hili tawi la Gor Mahia? Mazwazwa wameuliza kwanini huo mtaa haukuitwa jina la Mtanzania, na mimi nauliza mbona hili tawi halikuitwa jina la Mkenya?

Mbona kuna Wakenya wengi wanaweza kuenziwa na Gor Mahia na si Magufuli? Wapo waliouliza Wanyama kaifanyia nini TZ, nami nauliza Magufuli kaifanyia nini Kenya?

Cha ajabu walioshabikia jina la Wanyama lisitumike Tanzania ndio watakaoshangilia jina la Magufuli kutumika Kenya. Na hiyo ndio tafsiri halisi ya Unafiki.

By SAMBUKILE/JF

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad