17 Jul 2017

FAMILIA Yaelezea Chanzo cha Kifo cha Mke wa Waziri Mwakyembe

Linah Mwakyembe, aliyekuwa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison George Mwakyembe imeelezwa kuwa alifariki dunia kutokana na saratani ya titi ambayo imekuwa ikimsumbua kwa zaidi ya miaka miwili.

Linah aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alifariki dunia usiku wa Julai 15 na anatarajiwa kuzikwa keshokutwa, wilayani Kyela, mkoani Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji ya Familia ya Waziri Mwakyembe, Solomon Kivuyo nyumbani kwa marehemu Kunduchi Beach, Manispaa ya Konondoni, Dar es Salaam aliyesema hayo na kueleza zaidi kwamba marehemu ameacha mume na watoto watatu.

“Alikuwa akisumbuliwa na saratani ya titi kwa zaidi ya miaka miwili, na alishawahi kutibiwa hospitali za hapa nchini, India na hata Uturuki,” alisema Kivuyo ambaye ni shemeji wa Marehemu.

Kivuyo ambaye ni Mtumishi katika Ofisi ya Rais Ikulu, alisema kuwa baadhi ya ndugu wataanza safari leo kwenda Mbeya wakati wengine wakitarajiwa kwenda kesho tayari kwa maziko ya ndugu yao huyo.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger