17 Jul 2017

NUHU Mziwanda Kuula Kwenye Lebo ya Ali Kiba.......

MKALI wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ yupo kwenye hatua za mwisho za mchakato wa kuingia mkataba na ‘record label’ ya Rockstar4000 ambayo pia ina msanii, Ali Kiba.
Akichonga na Over Ze Weekend, Nuh alisema kuwa, haitakuwa busara kila kitu kikawekwa wazi kabla ya makubaliano ya kusaini lakini mashabiki wakae wakijua yupo njiani kujiunga na lebo hiyo.

“Ni kweli nipo kwenye mazungumzo na lebo ya Rockstar4000 ambayo yupo Kiba na soon nitasaini mkataba. Nimekubali kufanya hivyo kwa sababu Kiba ni mtu wangu wa karibu na ninamheshimu kama kaka yangu, naamini tutafanya kazi vizuri tukiwa pamoja huko na hakuna nitakacho-pungukiwa kwa kuminywa kivyovyote vile,” alisema Nuh.

Lebo hiyo pia ina wasanii wengine akiwemo Lady Jaydee, Ommy Dimpoz pamoja na Barakah The Prince.

Mayasa Mariwata

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger