Shilole; Nimepata Haja ya Moyo Wangu Tayari Nipo Kwenye Maandalizi Mazuri ya Ndoa Yangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Shilole; Nimepata Haja ya Moyo Wangu Tayari Nipo Kwenye Maandalizi Mazuri ya Ndoa Yangu
Msanii Shilole 'Shishi Trump' amefunguka kwa kudai yupo katika maandalizi yake ya mwisho ya kuolewa huku akiwasisitizia mashabiki zake kuwa safari hii hakuna maneno mengi kama zamani kwa kuwa amepata haja ya moyo wake.


Shilole amebainisha hayo baada ya baadhi ya mashabiki zake kutomuamini kwa kauli zake kwa kuwa mara nyingi ameonekana kuwa mwenye 'drama' nyingi katika mambo ya msingi anayowataarifu watu.
"Nipo kwenye maandalizi mazuri ya ndoa yangu lakini safari hii hakuna tena longo longo kama ambavyo 'sometimes' watu walivyozoea blah blah maneno mengi lakini mwanzo nilikuwa sijapata mahali pakufia lakini sasa hivi nimepata inabidi tu nikubali kufa", alisema Shilole.
Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kwa kusema "Mungu  akiamua kukuletea vitu vyake, anakuletea tu pale ambapo wewe hukutegemea wala kuwaza kama utapata. Unabaki kusema 'realy' hivyo haya yote ni mipango ya Mungu".
Kwa upande mwingine, Shilole amebainisha kuwa chanzo cha kukutana na mume wake mtarajiwa ni katika sherehe ya msanii Linah Sanga ya 'birthday' iliyofanyikia mjini Zanzibar na ndiyo hapo mapenzi mubashara yakaanza mpaka leo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad