Mfalme Mswati Ameoa Mke wa Miaka 19 Na Kuwa Mke wa 14

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mfalme Mswati Ameoa Mke wa Miaka 19 Na Kuwa Mke wa 14
MFALME Mswati wa Tatu wa Swaziland kwa mara nyingine ameongeza idadi ya wanawake kwa kuoa mwanamke mwingine. Katika kuadhimisha Ngoma ya Umhlanga ambayo hufanyika kila mwaka kwa kumpa mfalme fursa ya kuchagua mwanamke wa kuoa, mfalme huyo hivi karibuni alimchagua Siphele Mashwama mwenye umri wa miaka 19 kuwa mkewe wa 14.


Msichana huyo ambaye ni binti wa waziri Jabulile Mashwama katika serikali ya nchi hiyo, alipewa manyoya maalum mekundu ya ndege anayejulikana kama emagwalagwala ambaye huhusishwa na sherehe hiyo maalum ya kifalme. Mswati ambaye ana umri wa miaka 49 huchagua wanawake waliovuka umri wa miaka 19.

Pamoja na talaka kupigwa marufuku katika nchi hiyo ya kifalme, Mfalme Mswati amewahi kuwataliki wake zake watatu. Siphele ambaye ni mhitimu wa Waterford Kamhlaba World University College, alifuatana na Mfalme Mswati alipohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni.
Habari hiyo ilifichuliwa na msimamizi wa sherehe za kifalme, Hlangabeza Mdluli, aliyethibitisha kwamba Mswati alikuwa amefuatana na mkewe huyo ambaye kwa umri ndiye mdogo zaidi.

Wake wengine wa Mswati.
Wake zake wengine ni pamoja na: Inkhosikati LaMatsebula, Inkhosikati LaMotsa, Inkhosikati LaMbikiza, Inkhosikati LaNgangaza, Inkosikati LaMagwaza (ameachika), Inkhosikati LaHoala (ameachika), Inkhosikati LaMasango, Inkhosikati LaGija (ameachika).

Wakiwa kwenye sherehe za mwaka.
Wengine ni: Inkhosikati Magongo, Inkhosikati LaMahlangu, Inkhosikati LaNtentesa, Inkhosikati LaNkambule, Inkhosikati Ladube na Inkhosikati LaFogiyane. Mfalme King Mswati, anayejulikana pia kama Ngwenyama, yaani simba, anasemekana kuwa na watoto zaidi ya 13 ambao ni pamoja na binti yake mkubwa zaidi aitwaye Sikhanyiso, Sibahle Dlamini, Makhosothando Dlamini, Majaha Dlamini, na Tiyandza Dlamini.

Mswati akikagua gwaride.
Wengine ni Sakhizwe Dlamini, Saziwangaye Dlamini, Bandzile Dlamini, Lindaninkosi Dlamini, Mcwasho Dlamini, Temtsimba Dlamini na Temaswati Dlamini, among others. Baba yake Mswati, Mfalme Sobhuza wa Pili, alioa wanawake 70. Mswati amekuwa akishutumiwa kwa kujilimbikizia utajiri wakati watu wake wengi ni maskini.
Hivi karibuni, nchi hiyo ndogo ilitumia kiasi cha Dola milioni 2.2 (sawa na Sh. bilioni 5) kwa kununua magari ya anasa aina ya BMW 740i na pikipiki 80. Magari hayo yalikuwa ni kwa ajili ya viongozi wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrikca (SADC) waliyoyatumia kwa ajili ya mkutano wa siku mbili.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MWANAUME MASHINE

    ReplyDelete
  2. Tamaa za kishenzi na mambo yaliyopitwa na wakati ukiuliza nn utaambiwa ni utamaduni wakati yeye anajipendelea kuchagua mabinti wadogo wadogo awaoe hapi hapo raia wake wanateseka na maisha kuwa magumu siku hadi siku kiboko Africa mtu akiwa kiongozi badala ya kuwasaidia watu wake wapate maisha na hudumu bora wao wanawakomoa wananchi hao hao waliowafanya wafikie hapo walipo sasa it's a big pitty

    ReplyDelete

Top Post Ad