Baada ya sakata la dawa za kulevya, Wema aweka wazi mahusiano yake na RC Makonda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Tangu mrembo Wema Sepetu akamatwe kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya kwa kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mnamo mwezi Februari mwaka huu, Mrembo huyo hajawahi kumposti wala kumzungumzia kwa lolote kama alivyokuwa akifanya hivyo kipindi cha nyuma.


Watu wengi waliamini kuwa kitendo cha Wema Sepetu kutajwa na RC Makonda kwenye  orodha ya Wasanii waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya kuliondoa urafiki wao waliokuwa nao awali.


Sasa, Wema Sepetu ameamua kuwaonesha mashabiki wake kuwa hayo yote yameshaisha na kwa sasa amerudisha yake ya urafiki na RC Makonda kama ilivyokuwa zamani.

Hayo, ameyathibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha akiwa na RC Makonda na kuandika kuwa “Kila lenye mwanzo lazima mwisho uwepo“.

Hatua hiyo ya Wema Sepetu imeonekana kuwafurahisha mashabiki wake wengi wakimsapoti kwa maamuzi hayo. Pitia baadhi ya maoni ya mashabiki wake baada ya uamuzi huo


Kwa upande mwingine, mrembo Wema Sepetu bado anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi na kesi yake itasikilizwa alhamisi ya tarehe 14 Desemba, 2017. kunako mahakama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. What a pity. Ni kiongozi wa serikali namna hii. Ni aibu zidi ya aibu. Kuna professional hapa na maadili. Huu si ushangingi tu.Hadhi na utu wa kikazi ni upi.Wapi maadikli.

    ReplyDelete

Top Post Ad