Mwanamuziki XXXTentacion Afariki kwa Kupigwa Risasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamuziki wa nyimbo za rap Marekani XXXTentacion, ambaye alipata umaarufu kwa haraka kupitia albamu zake mbili ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa na miaka 20.

Alikuwa anaondoka kwenye duka la kuuza pikipiki kusini mwa Florida Jumatatu pale mtu mwenye bunduki alipomfyatulia risasi.

Polisi katika tarafa ya Broward wanasema XXXTentacion, ambaye jina lake Jahseh Onfroy, alikimbizwa hospitalini lakini akathibitishwa kufariki.

Alikuwa mara nyingi akielezwa kama mmoja wa wanamuziki wa rap wenye kuzua utata zaidi.

Alikuwa pia amekabiliwa na mashtaka ya kumshambulia mpenzi wake.

Rapa huyo, ambaye alipata umaarufu kwa kupakia nyimbo zake katika mtandao wa SoundCloud, alikuwa anatazamwa na wengi kama kielelezo cha mtu kufanikiwa kupitia kipaji chake.

Beyonce na Jay-Z watoa albamu pamoja, wamtaja Trump
Wapenzi wa muziki wake na wanamuziki nyota wa hip-hop wamekuwa wakituma salamu za rambirambi kuomboleza kifo chake.

Liwali wa tarafa hiyo amesema Onfroy alikuwa anaondoka kwenye duka hilo muda mfupi kabla ya saa kumi alasiri pale washukiwa wawili waliokuwa na silaha walipofika kwake.

Albamu ya karibuni ya mwanamuziki huyo ilianza ikiwa kwenye orodha ya nyimbo 200 bora Marekani
Mmoja wao anadaiwa kumpiga risasi kabla ya wote wawili kukimbia eneo la tukio Deerfield Beach, takriban maili 43 (69km) kaskazini mwa Miami wakitumia gari aina ya SUV la rangi nyeusi.

Wachunguzi wanasema huenda kilikuwa kisa cha wizi wa mabavu.

Video iliyopakiwa kwenye mitandao ya kijamii ilimuonesha mwanamuziki huyo akiwa amelala ndani ya gari lake baada ya kupigwa risasi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad