Nani ni Muhimu Katika Maisha yako? Soma Hichi Kistori Kifupi cha Kufundisha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Siku moja katika darasa la jioni la watu wazima, mwalimu wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi;

"Nataka tucheze mchezo, mtu yeyote yule naomba ajitolee aje hapa mbele"

Mwanamke aitwae Cathy akatoka mbele. Mwalimu akamwambia aandike majina 30 ubaoni ya watu ambao anadhani ni wa muhimu katika maisha yake.

Cathy akaandika majina ya wanafamilia yake yaani mumewe na mwanae, ndugu, majirani na marafiki zake.

Mwalimu akamwambia Cathy afute majina matatu ambayo anadhani kwake sio ya muhimu sana kuzidi mengine. Cathy akafuta majina ya marafiki zake watatu.

Mwalimu akamwambia Cathy afute tena majina matano zaidi, Cathy akafuta majina ya majirani zake watano.

Hii iliendelea mpaka alipobakiwa na idadi ya watu wanne tu katika ubao. Haya yalikuwa majina ya wazazi wake, mumewe na mtoto wake wa pekee.

Darasa zima wakabaki kimya, baada ya kugundua kuwa huu sio mchezo wa Cathy peke yake sasa.

Mwalimu akamwambia Cathy afute majina mengine mawili kati ya yale manne yaliyobaki. Ulikuwa uamuzi mgumu mno kwa Cathy. Bila hiyari akafuta majina ya wazazi wake.

"Futa jingine zaidi tafadhali" mwalimu alimwambia.

Cathy akaishiwa pozi, na huku mikono ikimtetemeka na machozi katika macho yake akafuta jina la mwanae wa pekee. Na kubakiza jina la mume wake, Cathy alilia mno!!!

Mwalimu akamwambia Cathy aende akakae. Baada ya muda kidogo mwalimu akamuuliza Cathy "kwanini mume wako? Wazazi wako ndio waliokulea na kukuza, Mtoto wako ndio huyo tu mmoja uliyenae!! Na unaweza ukapata mume mwingine!!! Kwanini??"

Darasa likawa na ukimya wa hali ya juu, kila mmoja akitamani asikie ni nini Cathy atajibu.

Cathy kwa ujasiri na utulivu akainuka na kusema, "siku moja wazazi wangu watafariki (Mungu anisamehe), mtoto wangu pia ataondoka pale atakapokua mkubwa kwenda kuanzisha familia yake.

Mtu nitakayebaki nae kumaliza nae maisha hasa uzeeni ni mume wangu tu!! Yeye ndiye niliyeunganishwa nae na Mungu, mimi na yeye ni mwili mmoja."

Wanafunzi wote wakasimama na kumpigia makofi kwa kushare nao ukweli na msimamo wa maisha yake.

Huu ulikuwa uamuzi wa Cathy, yeye kwa mtazamo wake alimchagua mumewe.

Je wewe ungechagua nani?
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hizi hadithi nyingine ni za kipuuzi sana,ni nani ajuaye kesho yake? Huyo mumewe anaweza kuwa wa kwanza kufa na hata wanawe na akabaki na wazazi wake ndio wakamsaidia yeye na kuwaacha lakini hata kama itakuwa kama hivyo alivyofikiri yeye ana uhakika gani akishakuwa hajiwezi iwe kwa maradhi au lingine lolote huyo mume akamkimbia na kumtelekeza abaki akiwakumbuka wazazi wake.

    ReplyDelete
  2. KWANI MUME HAWEZI KUFA? NANI KAKWAMBIA MUME WAKO UTAISHI NAYE MPAKA UZEEKE? WEWE NI MUNGU? MOTHER F****CK***

    ReplyDelete

Top Post Ad