MSHUKIWA WA DAWA ZA KULEVYA ALIYE TAJWA NA MWAKYEMBE!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe amemtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga, lakini mshukiwa huyu pamoja na picha zake alishaandikwa na gazeti la SANI katika toleo lake la Agosti 7-9, 2013 (toleo la 1042) pamoja na namna alivyosafirisha mzigo pamoja na akina Masogange.

Isome taarifa yao:

Na Mwandishi Wetu
Unaweza kukimbia lakini huwezi kujificha. Msemo huu unaonekana kutimia kwa kijana anayedaiwa kuambatana na watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa Julai 5 mwaka huu nchini Afrika Kusini, Agness Gerald 'Masogange' (25) na Melisa Edward (24), kunaswa na gazeti hili.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, wasichana hao, Masogange na Melisa walisafiri ndege moja na kijana anayejulikana kwa jina la Nassoro Mangunga wakitoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini, wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), yenye namba SA 189.
Wakiwa katika ndege hiyo Mangunga, Agness na Melisa walikaa kwenye viti vilivyo jirani kabisa huku Mangunga akiwa katikati yao, kwani Agness alikaa kiti namba 23B, Mangunga alikaa kiti namba 23D na Melisa alikaa kiti namba 23A.
Mangunga ambaye ni rafiki mkubwa wa wanamuziki wa Bongo Flava, Rashidi Abdallah Makwiro 'Chid Benz', Mgaza Pembe 'M2theP' na Albert Keneth Mangweha 'Mangwair', wakati akisafiri na mabinti hao walikuwa na jumla ya mabegi tisa kama kumbukumbu za nyaraka za shirika hilo la ndege zinavyoainisha.
Licha ya nyaraka za kusafirishia mabegi hayo kuonesha jina la Agness Gerald ambaye ni mpenzi wa Mangunga tangu mwanzoni mwa mwaka jana, kuwa ndiye aliyelipia mabegi hayo, ila kwenye sehemu ya anuani ya waraka pepe, imeandikwa ya Mangunga (inahifadhiwa) ya tovuti ya Gmail.
Aidha, mabegi hayo, yalikuwa na kilo 150 za dawa za kulevya lakini kila mmoja alitakiwa kusafiri na kifurushi cha kilo ishirini kama mzigo wa mkononi ambao husafiri bila malipo, hivyo watatu hao kwa pamoja walikuwa na kilo sitini wote kwa pamoja, hivyi kubaki kilo 90 ambazo walizozilipia Dola za Marekani 94 badala ya Dola 450.
Mangunga ambaye licha ya kuishi zaidi nchini Afrika Kusini, lakini pia ni mkazi wa maeneo ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Agness na Melisa, walikamatwa Julai 5, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo, Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8 za Kitanzania, na walipotiwa mbaroni, walikuwa na mabegi sita tu kati ya tisa waliyokuwa nayo wakati wanapanda ndege jijini Dar es Salaam.
Inasemekana mabegi hayo matatu yaliondoka na Mangunga na kutokomea kusikojulikana, jambo linalolifanya Sani kuzamia zaidi ili kuweka mezani timu nzima inayohusika na mzigo huo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

28 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aliyepeleka majina ni mange kimambi .mange allitaja majina Mpaka la mume wa shamim Kwenye blog yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. jamani wewe anonymous mbona una dhambi hivyo. mange kimambi wala hakujata jina hata moja usimsingizie mtoto wa watu. hizi chuki nyingine haziwapeleki popote,. mnazidi kujitafutia shida tu na kuwa haters. get a life please.

      Delete
    2. Kweli alitaja ila akisema ni wauza sembe akasema watu wakamuonya akasema ye hajasema madawa ya kulevya kasema sembe..

      Delete
    3. Mange na gazeti la sani ndio wenyewe.Alimtaja mume wa shamim na aliendelea .wewe Unafikiri ni vizuri kutaja mume wa Mtu bila evidence Ona sasa Watu wanavyokamatwa .Na mange aliandika " anasikitishwa na hao Watu kwa sababu anawajua na haamini wamefanya hayo mambo na hao Watu wanamaisha mazuri " . Unajua unaweza sema Kitu au andika Kitu yaks kutokea puani .Alimuona mume wa shamim Akiuza madawa alikamatwa leo na mwakyembe mange anaushahidi gani ??!

      Delete
    4. Jamani mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni khaa! Mange lini kamtaja mtu jamani!? Sasa chuki zenu zimevuka mipaka na Mungu hapendi.

      Kwa hiyo huyo mtu kujulikana na watu wauza unga kujulikana nimakosa! Angalieni vijana wanavyo athirika na madawa ya kulevya..badala ya kufurahi kwa watu kujulikana na wachukuliwe hatuwa nyie ndio kwanza mnazusha story zingine ohh mange this mange that! Embu muogopeni Mungu

      Delete
    5. Wewe Kama si Linda ni wauza nguo wenzie ambao wanaoneana wivu kila kukicha tena uliyeandika hii comment ulaaniwe wewe na kizazi chako chhote,unajua wazi wauza sembe hawanaga Mungu,unaandika Hivi ili mange auwawe?lini kawataja wauza sembe kwa mwakyembe?na hayo Mabarua ya hong kong mange ndie kaandika?Yore ni chuki Kwakuwa mwenzenu kawazidi.?chuki tu Kama mnamchongea afe na nyinyi mtamfuata.yani mijanamke Ina roho mbaYaaa,yaani mwanamgu nitamuhusia asiwe na rafiki du.

      Delete
  2. inaweza kuwa maana gazeti la sani na mange zinaiva alilitumia kumchafua linda kupitia gazeti la sani

    ReplyDelete
  3. Huyo ni shetani,na chuki zako zisizo na kichwa wala miguu,mange hakutaja hata jina la mtu mmoja acha unafki,msonyoooooooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. kaaaz ipo kwan hata kama kataja kuna nini

      Delete
  4. Umedai walikuwa na mabegi 9,yenye kilo 150 na kilo 60 walibeba ktk hansbag ili wacliopie,90 zikabk ktk mabeg,je huyo nasoro alto na mzga gan wakat hao wadada wamekutwa na kilo 150 zote? Inamana huyo aliacha mizgo yake?

    ReplyDelete
  5. vigogo waserikali mbona hawakutajwa hapo au.ndo mabo..c zake

    ReplyDelete
  6. Mwakyembe ni DR sio PROF,kuwa makini unapoandika habari zako.

    ReplyDelete
  7. Watajwe na mapapa basi hao vidagaatulishawajua kitambo kabla hawajakamatwa tunaishi nao kitaa tunajua inshu zao ni unga ila kuna mabosi wao hiyo mipapa ndio tunaitaka sisi.

    ReplyDelete
  8. Mapapa wanawaogopa kwani hawawajui,ila kwa mwakembe tutawajua

    ReplyDelete
  9. Jamani hayo mambo serious .Ni kweli mange ndio source na wengine aliwataja kwa sababu ya wivu wake tu .muongooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. aliwataja wapi? huyo mume wa Shamimu ni kweli anauza sembe. nani asiyemjua magomeni. Hebu acheni chuki zisizokuwa na tija. hao wauza sembe wote wakamatwe. kuanzia vidagaa hadi hao mapapa. msitake kumsingizia mtoto wa watu. yeye aliweka tu post sema watu ndiyo wakawa wanacomment. na watu wanaocomment wanamfahamu fika Abdul Nsembo mume wa Shamimu Mwasha. Huyo shamimu na wadada wote wa mjini waache tamaa na kupenda vitu vikubwa wakati hawana uwezo. wanaishia kwenda kwa wauza semba!!! llooh na iko siku tu hao wauza sembe wote watakamatwa mmoja baada ya mwingine.

      Delete
    2. Uwe na evidence mange

      Delete
  10. Mange CCM ndio pake .Anania ya kugombania

    ReplyDelete
  11. Awe na evidence Hipi? Kwani true ndie aliyetaja?Mensa kwenye list ya hongkong Kama hutakuta Abdul choji,Hilo jina nail nickname yake.msimsingizie mange wa watu,eee bedui wewe na wauza nguo,mlaaniwe na vizazi vyenu vyooooote.

    ReplyDelete
  12. Kuna mdadas Anaitwaflaviana mi simpendi,Kutwaaa dar kuchonganisha watu,shughuli zone za wadada wa MUJi yumo,akosekani.Jana watu walikuwa wanamzungumzia pale rose garden,eti ndio mkaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanawake mna wivu kutwaa Kelele

      Delete
  13. Hee na yule mdada anayeitwa kisa,Sikuhizi anajiita Kiki Yani ni baraa mswahiliiiiiili mpaka kichefuchefu,kutwa kutwaa kupita picha kwenye mahoteli,ndio maana akamsimamia Ndoa mswazi mwenzie mange.ndoa Hana kazi majungu na mwamvita makamba,mijitu inajitia misomi Kumbe upupu mtupu,hao wote hawanaga Ndoa wameachika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mange kimambi ndio alitoa list ya majina .Habari ndio hiyo mjini ndio maana alikuwa anawaambia anaogopa kumwagiwa TINDIKALI .

      Delete
    2. Topic imegeuka Kuwa mange na maugomvi yake .watu kaeni Kwenu mtulie na family zebu duh .

      Delete
  14. Sasa mnachotaka umu mume wa shamimu mwasha,mr Abdul chonji amuue mange?mume wa shamim jamani mi Naomba muende magomeni mkamuulizie,always mesa kweli anaonekana mzushi ka mwakyembe,kwenye msiba wa mange Mungu Apishe mbali wauza nguo na wapambe mnaomchukia ndio mtajazana.Afi ng'ooooo mtakufa nyie na roho zenu mbaya.

    ReplyDelete
  15. Linda bedui Linda bedui Linda bedui how many times have I called you?wewe una 43 years,halafu unadanganya watu una 41,don't act like mwanao leila,umekuwa bibi,mange umempita miaka kumi,ebu muache apumue,taffeta kazi ya kukukeep busy

    ReplyDelete
  16. kweli watanzania bado tupo nyuma sana. Tunapenda kujadili watu, huyo kaka anajulikana biashara anayofanya. Kumtaja mhalifu sio mbaya kama unamuhisi ili jamii itambue na polisi kufanya uchunguzi. Vijana wengi wenateketea kwa madawa ya kulevya wakiwemo watoto wetu, kaka zetu,dada zetu na hata baba zetu. Kikubwa ni kukaa na kufikiri kwa jinsi gani tutasaidiana kupambana na tatizo la madawa ya kulevya kuwaokoa ndugu zetu. itafika wakati tutaanza kulipana visasi kwa kuwaharibu watoto wa hao wafanyabiashara kwa kutumia hayohayo madawa wanayouza wazazi wao kama wanavyowaharibu watoto wetu

    Ndugu zangu, inauma sana ukiangalia vijana walioathirika na madawa hayo

    ReplyDelete
  17. Kama wametajwa serikali iswakalie kimya wafuatiliwe na ukweli ujulikane mambo ya kuleana yaishe , sio kusubiri na kuwa na Taifa la wauza unga . Na nadhani serikali au kwenye katiba ijayo tuweke sheria mama anayekamatwa na madawa ya kulevya auawe tena kwa risasi.

    ReplyDelete

Top Post Ad